Na
Hadija Hassan, Lindi.
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi inawashikilia
viongozi 51 wa vyama 10 vya Msingi vya (AMCOS) vinavyodaiwa na wakulima wa
Ufuta wa Mkoa huo kiasi cha Shilingi milioni 486, 869,982 za Msimu wa Mwaka
2019.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya Habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia John Mbungo leo Oktoba 17,
kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo Mkoani Lindi alisema kuwa ukamatwaji wa viongozi
hao wa vyama vya Msingi ni utekelezwaji wa maagizo ya Mh, Rais Dkt, Pombe
magufuli.
Alisema
Rais Magufuli aliyoyatoa maagizo Oktoba
15, 2019 katika mkutano wa Hadhara na Wananchi wa wilya ya Ruangwa Kupitia
hadhira hiyo Rais Magufuli aliimtaka Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Nchini
Brigedia Mbungo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe , kuhakikisha
kuwa vyama kumi vya Msingi (AMCOS) vinavyodaiwa na wakulima wa Ufuta vinalipa
fedha hizo kabla ya Msimu wa Korosho kuanza.
Mbungo
aliwataja viongozi hao walioshikiliwa na Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na Hemedi
Yasini kilete – Mwenyekiti , Saidi Hemedi Mkwela – katibu, Twahili Kileta –
karani, Hillard Cosmas Chadill – Karani na Hassan Lidemu – Karani wa Chama cha
Msingi cha Milindimo AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni 90,711,354.00
Hasani Lingunja – Karani, Karimu Ngara – Karani wa chama cha Msingi cha Mtonao
AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 73,715,760.00.
Wengine
ni Zuber Omary Nolele – Mwenyekiti, Mjamari Haji Kibohu – Katibu wa Chama cha
Msingi Kipelele AMCOS Kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni 57,257,280.00,
Hussein Ally Mnindi – katibu wa Chama cha kinjikikitile AMCOS Saidi Mohamedi
Mbunda- Makamu Mwenyekiti, Mathiad Mohamed Likumwili – mjumbe, Chande Mshamu
Madudu – mjumbe , Issa Lutumno – mjimbe, Nasra Chingwile karani wa chama cha
msingi nachiunga AMCOS kwa kudaiwa shilingi millioni 10,780,100.00.
Ameendelea
kuwataja wengine kuwa ni Abdallah Athumani Mtala – Mwenyekiti, Karimu Bakari
Maguto – katibu, Hussein Saidi Hussen – Mjumbe, Latifa Abdallah – Karani ,
Amina Issa Mtauna – Mjumbe wa chama cha Msingi Chikonji AMCOS Kwa kudaiwa kiasi
cha Shilingi Milioni 10,325,550.00.
Viongozi
wengine ni Zainabu Khalifa - makamu mwenyekiti, Bashiri ally – katibu ,
Abdallah Abdallah – katibu Msaidizi , Haji juma Namanyanga – Karani, Mohamed
Abrahaman Ligoli - Karani, Saidi hashi Nguli – Kalani, Pius Lucas – Karani,
Abrahamani Mohamedi Kapanda – Karani wa chama cha Msingi cha Mtama AMCOS
kinachodaiwa kiasi cha Shilingi Milioni 8,523,830.00 pamoja na shilingi
160,00.00 za Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao.
Aliendelea
kuwataja wengine kuwa ni Ally Kinyemela Mtombo – Katibu, Mshamu Mohamedi
Ngurangwa – Karani wa Chama cha Msingi Matumbi AMCOS Nurdini Ndope –
Mwenyekiti, Shaibu Matumbi – Katibu, Hamza Kumtitima – Katibu Msaidizi Mustafa
Chumbo- Mjumbe, Selemani Mtonda – mjumbe, Mponjila Bakari Mponjila karani wa
Chama cha Msingi Ruangwa – Mandawa AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha shilingi milioni
4,095,200.00,
Mussa
Maringa – Mwenyekiti, Jafari Saidi Likwena – Makamu Mwenyekiti, Patrick Martine
– Katibu, Abdallah Maringa – Mjumbe Mjumbe wa Bodi, Hassan Mteremko - Karani wa
Chama cha Msingi Mchina AMCOS kwa kudaiwa Shilingi milioni 3,604,500. Isumail
Mkopi – Mwenyekiti, Hamida Kaulu – Makamu Mwenyekiti, Masoud Hamisi – Katibu,
Nadhifu Nauka – Katibu Msaidizi, Isumail Nauka – Mjumbe wa Chama Cha Msingi
Mnolela AMCOS kwa kudaiwa na wakulima kiasi cha Shilingi Milioni 3,052,000.00
na Said Mchia – Mwenyekiti, Aziz Mchemba – Katibu, Abubakari Maharagwe – Mjumbe
wa chama cha Msingi Mmangawanga AMCOS kwa kudaiwa na wakulima kiasi cha
Shilingi milioni 3,314,300,00.
Saidi
Nyalubi Mpili – Mwenyekiti, Saidi Likotea – Katibu, Bakari Mpili – Mjumbe wa
Chama cha Msingi Mageuzi AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni
2,630,000,00 Hata hivyo mbunga alisema kuwa kati ya fedha shilingi milioni
436,869,982 zinazodaiwa na wakulima hao wa Ufuta tayari watuhumiwa hao
wamesharejesha kiasi cha Shilingi milioni 46, 416,830,00.
Mbunga pia alisema
kuwa zoezi la ufuatiliaji wa madeni ya wakulima litaendelea kwa AMCOS za
Nyangamara, Namangle, Nahuka huku, Mtua, Kigoli, Malungo, Madwanga, Nanjilinji,
“A”, Zinga, Rutamba, Nyangamara, Naambu, mbwemkuru, Mlindimo Mtunaho AMCOS
Mbunga pia alitoa rai kwa viongozi wote wa vyama vya ushirika Nchini
vinavyodaiwa na wakulima viwalipe wakulima hao haraka iwezekanavyo kabla ya
TAKUKURU haijawafikia huku akisisitiza kuwa katika zoezi hilo hakutakuwa na
chama ambacho kinadaiwa kitakachobaki salama
No comments:
Post a Comment