Mbunge
wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akikabidhi hundi kwa Kudura Selemani kutoka kikundi cha Ushirika.
........................................
........................................
Mbunge
wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, amegawa fedha zaidi ya
milioni 31 kwa vikundi na taasisi katika jimbo hilo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi fedha hizo Dkt. Kawambwa alisema kuwa, fedha ni zile za
mfuko wa jimbo ambazo zipo kisheria na zinatolewa na serikali kwaajili ya
kusaidia mambo mbalimbali katika jimbo husika.
Alisema
fedha hizo alizogawa ni jumla ya 31, 801,000 ni kwaajili ya kuchochea maendeleo
kwa vikundi vya wajasriamali na taasisi ambazo hazipaswi kurudishwa.
Aidha,
alitoa wito kwa wananchi wa jimbo la Bagamoyo, kujiunga katika vikundi ili
weweze kuwa na sifa ya kupata fedha za mfuko wa jimbo na zile asilimia kumi
zinazotolewa na Halmashauri.
Alisema
serikali imetenga fedha kwaajili ya kuwezesha wananchi katika maeneo mbalimbali
ambapo ili uweze kupata fedha hizo ni lazima muwe katika kikundi.
Alifafanua
kuwa, serikali haiwezi kugawa fedha kwa mtu mmoja mmoja ispokuwa fedha
zitatolewa kwa vikundi ili iwe manufaa kwa watu wengi zaidi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa amewataka
wanavikundi na taasisi zilizopata fedha hizo kuzitumia katika malengo
yaliyokusudiwa ili zilete tija kwenye
jamii.
Alisema
ni kweli fedha hizo hazitarudishwa lakini vikundi vitapitiwa kukaguliwa ili
kujiridhisha kuhusu matumizi ya fedha hizo.
Kwa
upande wao wanavikundi waliopata fedha hizo wamemshukuru Mbunge Dkt. Kawambwa
kwa kupatia kiasi hicho ambacho kitasaidia katika kusukuma maendeleo kwenye
maeneo yao.
Walisema
serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijali watu wa aina zote na ndioamana fedha
hizo zimewafikia jambo ambalo hawakulitarajia.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akikabidhi hundi kwa Golden Mwenda Magagula kutoka kikundi cha Unjacha.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza na wana vikundi katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa, na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya hiyo, Fatuma Omari Latu.
Kutoka
kulia ni Diwani wa viti maalum, Hapsa Kilingo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Ally Ally Issa, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne
Kawambwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Omari Latu,
Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela, na Amina Ramadhani.
Diwani
wa kata ya Zinga, Mohamedi Mwinyigogo (kulia) akiwa na Diwani wa viti Maalu, Shumina Rashidi, wakimsikiliza katibu wa Mbunge, Magreth Joseph aliyesimama.
No comments:
Post a Comment