Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo akiongea wakati wa kufunga
Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii
lilofanyika jijini Dodoma.
........................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jafo ametao mwezi mmoja kwa
Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinafungua akaunti maalum ya Benki kwa
ajili ya fedha za maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo jana
wakati akifunga kongamano la wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii jijini
Dodoma nakuwataka wataalam hao kuhakikisha wanakwenda kusimamia zoezi hilo na
kukamilisha katika kwa kipindi cha mwezi mmoja.
‘’Natoa maagizo ifikapo Novemba, 30 kila
Halmashauri Nchini iwe imefungua akaunti maalum ya Benki kwa ajili fedha ya
wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwa fedha zikitolewa katika mfumo
wa sasa zinakuwa kama zinaelea’’. Alisitsiiza Waziri Jaffo.
Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa
fedha hizi zinapotelewa bila akaunti hiyo inakuwa vigumu kwa serikali
kuzifanyia tathimini hivyo kuwaimiza wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii
katika Halmashauri zao kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili malengo na
matumizi ya fedha hizo yaweze kufanyiwa tathimini.
Pamoja na kutoa agizo hilo Waziri
Jafo pia ameongeza kuwa ili jamii iweze kuleta mabadiliko yanayotakiwa suala la
kutumia wataalam wa maendeleo ya jamii halikwepiki kwa sasa wakati jamii
inataka mabadiliko ya haraka kuelekea Tanzania ya viwanda.
Wataalam hawa ni chachu ya mabadiliko
na katika mashirika makubwa duniani wataalam wa maendeleo ya jamii wamekuwa
wakitumiwa sana ili kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali na wamekuwa
msaada mkubwa kitaifa na kimataifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika hotuba yake kwa Waziri huyo aliongeza
kuwa kongomano hilo lilikuwa na mjadala mkubwa kuhusu kuhamasisha jamii
kujiletea maendeleo kwa kutumia istilahi zilizoko katika jamii
akitolea mfano wa istilahi maalufu kwa mikoa ya ya kati ijulikanayo kama
Msalagambo.
Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa
matokeo ya kongamano hilo pia nikuwafanya wataalam hao wajione kuwa wao ni
chachu ya maendeleo katika kuhamasisha wananchi kuwa na ari ya kujiletea
maendeleo.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Sera na
Mipango kutoka TAMISEMI aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara yake katika
Kongomano hilo Bw.John Miayo Cheo aliwataka wataam wa maendeleo ya jamii
kutumia taaluma yao kuhamasisha wananchi kugombea nafasi za uongozi ili waweze
kuwa viongozi wa kufuatia uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.
Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya
Jamii wamekutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la
kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada
mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne
No comments:
Post a Comment