Wednesday, October 30, 2019

TGNP kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa nchini

TGNP Mtandao imepanga kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa kwa mrengo wa kijinsia na kushauri kufanya marekebisho mapema kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Viongozi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao kutoka TGNP Mtandao, wakionesha Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2019 iliyotengenezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki za wanawake.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukabidhi ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa chama cha ACT wazalendo,  Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao  Lilian Liundi, alisema kwamba baada ya kutembelea vyama kadhaa vya siasa nchini na kusikiliza jinsi wanavyotekeleza masuala ya kijinsia, ameona kuwa kuna haja ya TGNP na Mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na Usawa wa Jinsia, kufanya uchambuzi au mapitio ya sera na ilani za vyama kwa mrengo wa kijinsia na kuangalia mapengo ili kushauri marekebisho.
“Tunapoelekea uchaguzi wa seriali za Mitaa,  na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2020, tunahitaji vyama hivi kuzingatia kwa kiasi kikbwa usawa wa kijinsia kwenye uteuzi wa wagombea. Kama chama hakina sera za ndani ambazo zina mrengo wa kijinsia, ni lazima mapendo yataendelea kuwepo. Tunashukuru kwamba vyama  vya siasa vimejitahidi, lakini bado hatujafikia malengo” Alisema.
Kwaupande wake Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Doroth Sembu alisema kwamba, pamoja na kwamba chama kinajitahidi kutoa fursa sawa kwa wanawake bado watajitahidi kuendelea kuteua wanawake kushiriki kwenye chaguzi.
“mwaka huu tumejipanga kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, tutahakikisha kila mahali ambapo wanawake wamejitokeza wanapata nasi, lakini kwa sababu mmetuletea hii Ilani yenu, tutahakikisha tunaitumia  ili wagombea watakao shinda wakatekeleze ilani husika” alisema Semu
Ilani ya Madai ya wanawake kwa  uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Mtandao wa wanawake na Katiba, imewashirikia na kukusanya maoni ya wanawake kutoka katika makundi yote nchini hasa vijijini. Asasi za kiraia zinazotetea haki na usawa wa Kijinsia zaidi ya 60 zimeshiriki.

No comments:

Post a Comment