Na Shushu Joel
Umoja
wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani umempongeza Rais wa jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyojali wanawake
katika teuzi mbalimbali pia katika utekelezaji wa miradi mikubwa kwenye Sekta
mbalimbali ikiwemo Afya inayolenga kumsaidia Mwanamke moja kwa moja.
Akizungumza
katika kongamano la maadhimisho ya wiki ya UWT iliyohitimishwa wilayani Kibiti
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Bi Farida Mgomi amesema kuwa Rais Magufuli
amekuwa kiongozi mwenye kuwaamini na kuwapatia nafasi mbalimbali wanawake
katika serikali ili waweze kumsaidia kusimamia shughuli za maendeleo kwa ajili
ya wananchi.
Alisema
mkoa wa Pwani umekuwa na wanawake shupavu na wenye kujitoa katika kuwahudumia
wanyonge na ndio maana wengi wamepata nafasi Serikalini na Chama pia.
"Umoja
wa wanawake mkoa wa Pwani tunampongeza sana Mhe Rais na Mkiti wa Chama cha
Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia wanawake nchini nafasi, na
kiukweli tunaona wanavyochapakazi na hawajamuangusha Mhe Rais na tunaahidi
kumuunga mkono katika uongozi wake "Alisema Mgomi.
Aidha
Mwenyekiti huyo amewataka wanawake kuendelea kuwa kinara wa upigaji kura
kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Kujiandikisha kwa wingi katika daftari la Ukaazi na la wapiga kura na
kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali.
Kwa
upande wake, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani ambae pia ni Naibu Waziri wa
Nishati Mhe. Subira Mgalu amewapongeza wanawake wa mkoa wa Pwani na nchi nzima,
kwa uchapakazi wao na kupelekea kuonekana katika ngazi za juu ya serikali na
hata kupata uteuzi.
Mbali
na hilo Mgalu amewahakikishia kinamama hao kuwa serikali ya awamu ya tano ipo
makini katika utekelezaji wa ilani kwenye Sekta zinazogusa maisha ya kila siku
ya wananchi wa kawaida hususan Kina Mama mfano wa Afya , Maji , Kilimo ,
Nishati , Ardhi nk.
Aidha
Mgalu ametoa doti za kanga 800 katika kila wilaya za mkoa wa Pwani ili kuuzwa
kwa wanachama wenye kipato cha chini ili nao waweze kupata sare hizo kwa bei
nafuu na waweze kuendelea kukitangaza Chama na UWT, pia uwe ni mradi rasmi wa
Jumuiya hiyo ili iweze kujiendesha.
Nae
Mbunge mwingine wa Viti maalum Mkoa wa Pwani, Mhe Zainabu Vulu, alisema kuwa wanawake ni
jeshi kubwa lenye mshikamano mkubwa na lenye uwezo wa kufanya maamuzi.
Vulu
aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za vijiji na mtaa amewataka wanawake
kujitokeza kwa wingi ili kukipigia kura za ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ili wapinzani waendelee kuisoma namba.
Aidha,
alisema kuwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi, CCM itashinda kwa
kishindo na hii ni kutokana na utekelezaji wake wa ilani ya Mwaka 2015 ambayo
imelenga kuletea maendeleo kwa wananchi .
Katika
hatua nyingine Waheshimiwa Zainabu Vulu Ma Subira Mgalu walitoa Seti moja ya
Kompyuta na (Printer) ikiwa ni hatua ya mwisho kumalizia utoaji wa Kompyuta na
Printer ambapo umefanyika kwa UWT wilaya zote nane za Mkoa wa Pwani lengo
likiwa ni kuimarisha utendaji wa jumuiya hizo.
No comments:
Post a Comment