Na
Alodia Dominick, Bukoba.
Waendesha
pikipiki katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameanza kuishi kwa wasiwasi
baada ya kuzuka watu wanaojifanya ni abiria kumbe wana nia ya kuwajeruhi na
kuwanyang'aya pikipiki zao nyakati za usiku.
Mmoja
wa majeruhi hao ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera
Bukoba Celvin Felix amesema, ilikuwa majira ya saa mbili usiku mwanzoni mwa
wiki hii akiwa amempeleka mteja wake katika eneo la Kagemu kata ya Kitendaguro
katika manispaa ya Bukoba mteja huyo alipomfikisha eneo alipokuwa anashukia
alimgeuka na kumkata na kitu chenye ncha kali kiganja cha mkono wa kushoto na
sehemu mbalimbali za mwili kisha kuondoka na pikipiki yake.
“Nilimbeba
mteja majira ya usiku akaniambia anaenda eneo la Kagemu lakini sikuwa na
wasiwasi kuwa anaweza kuwa mwizi tulipofika alipokuwa anashukia bahati mbaya
kalikuwa kama ka poli nyumba ilikuwa mbele kidogo kusimama tu nilishutukia
ananikata panga la mkono kabla sijajiweka sawa alinikata sehemu nyingine za
mwili ndipo nilianguka na kuachia pikipiki na huyo mwizi kuondoka na piki piki
yangu”.
Alisema
Felix Felix ameendelea kusimulia kuwa, baada ya kupiga kelele za kuomba msaada
ndipo wasamaria wema walifika na kumkimbiza hospital ambapo anaendelea kupata
matibabu.
Kamishna
msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kuwepo
kwa matukio hayo na kusema kuwa, pikipiki zipatazo 14 zimeripotiwa kuibwa
mkoani Kagera kati ya septemba 11 mwaka huu hadi octoba 20 mwaka huu.
Malimi
amesema kutokana na taharuki hiyo jeshi la polisi lilijipanga na kuanza msako
na kubaini kuwa kuna kikundi cha wahalifu ambacho kimeanzishwa na mtu mmoja
ambaye alitoka mahabusu hivi karibuni na katika msako huo watuhumiwa wawili
ambao ni Amdani Mswadiko (27) mkazi wa kata ya Katoro halmashauri ya Bukoba na
Godwin Julius (31) mkazi wa manispaa ya Bukoba wamekamatwa pamoja na pikipiki
nne zimekamatwa katika msako huo.
Kamanda
Malimi amezitaja pikipiki zilizokamatwa katika msako huo kuwa ni pamoja na
Bajaji Boxer mc 937 BRL, ya pili ji Bajaji Boxer mc 845 ASL, ya tatu ni Babjiji
Boxer mc 632 BSU na ya nne ni Bajaji Boxer mc 570 BFA.
Hata
hivyo amesema katika msako huo pia waliwakamata watu saba ambao wanadhaniwa
kuwa wezi wa n’gombe ambapo n’gombe walioripotiwa kuibwa walikuwa ishirini na
waliokamatwa katika msako ni saba.
No comments:
Post a Comment