Tuesday, October 22, 2019

TPDC YAWEKA MPANGO WA KUWASAIDIA WANANCHI KWA KUWA NA MRADI WA GESI ASILIA

Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa maonyesho ya  bidhaa kwa wawekezaji wa viwanda Mkoa wa Pwani (PICHA VICTOR MASANGU).
.................................................
 

VICTOR MASANGU, PWANI


SHIRILA la maendeleo ya petroli  Tanzania  (TPDC) katika kukabiliana na changamoto ya uagizaji wa mafuta  kutoka nje ya nchi imekuja na mpango kabambe  wa  miradi mikakati mitatu  kwa ajili ya kufanya utafiti  wa uchimbaji wa visima vya mafuta  katika mikoa ya Tabora, Simiyu, pamoja na singida lengo ikiwa ni kuipunguzia serikali ya awamu ya tano  kutumia  gharama kubwa  katika  suala zima la uagizaji.


Hayo yalibainishwa na Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya wakati wa  maonyesho ya bidhaa za  wawekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani, ambapo pia amebainisha kuwa lengo lao lingine ni kuweza kutanua wigo katika kuzalisha gesi asilia katika maeneo mbali mbali nchini ambayo  itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kuondokana na matumizi ya ukataji wa miti ovyo.


Kwa upande wake Afisa uhusino wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Latifa Kigoda amesema kwamba lengo kubwa ni kuwasimamia na kuwaunganisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ikiwemo kutanagaza fursa mbali mbali zilizopo kwenye kilimo pamoja na kuongeza thamani katika mazao ya biashara sambamba na kuwa na vifaa tiba ambavyo vinazalisha ndani ya nchi.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye amepokea jopo la wawekezaji  saba Kutoka jimbo la hebeyi la nchini  China, na kuwakabidhi mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa ambao utaweza kuonyesha fursa mbali mabli ambazo zinapatikana katika halmashauri zote tisa lengo ikiwa ni kuwapatia maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa kuzalisha chuma, nondo na saruji.

No comments:

Post a Comment