Kiongozi
wa mbio za Mwenge kitaifa 2019 mzee Mkongea Ally akiwasalimia wananchi wa mtaa
wa mto mkavu kata ya Mbanja wakatai makabidhiano ya Mwenge huo kati ya
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na Halmashauri ya manispaa ya Lindi Mkoani humo.
..............................................
NA HDIJA HASSAN, LINDI.
Mwenge
wa Uhuru uliokuwa unakimbizwa wilayani Kilwa Mkoni Lindi umemaliza mbio zake na
kukabidhiwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally amesema miradi mitano ya maendeleo
iliyopangwa kuzinduliwa wilayani humo, imeridhiwa na wataalamu wake.
Akizungumza
na wananchi waliojitokeza kupokea mwenge huo leo asubuhi (jumapili, Oktoba 13,
2019) kwenye mtaa wa mto Mkavu kata ya Mbanja halmashauri ya Manispaa ya Lindi,
Mkongea aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kuwa na miradi mizuri
sambamba na kuwataka viongozi wa Manispaa ya Lindi kuhakikisha wanakuwa na
Taarifa zote muhimu kwenye kila mradi utakaopitiwa na mwenge huo wa Uhuru
sambamba na kuwataka wataalamu kuwa katika maeneo yao ya Miradi.
Mkongea
pia aliwataka Viongozi kusimamia maadili pamoja na itifaki za mbio za mwenge wa
Uhuru zinazotolewa na wakufunzi husika kwani Mwenge huo wa Uhuru sio wa
mkimbiza Mwenge bali ni uwakulishi wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
na tunu ya muasisi wa Taifa Mwalimu Julias kambalage Nyerere hivyo ni wajibu wa
kila mtu kukiheshimu chombo hicho muhimu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya kilwa Christopha Ngubiagai aliitaja miradi
iliyopitiwa na Mwenge huo wa Uhuru ni pamoja na kutembelea na Kukabidhi mikopo
kwa vikundi vya wajasiriamali katika kijiji cha Njinjo, kuweka jiwe la msingi
Duka la Dawa na Chumba cha kuhifadhia maiti, kuzindua Mradi wa maji katika
kijiji cha Mpara, kutembelea Mradi wa Barabara Masoko pamoja na kuweka jiwe la
msingi katika Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Madarasa na Bwalo la chakula
katika Chuo cha wananchi Kilwa Masoko ambayo inathamani ya shilingi bilioni 1
na milioni 900.
Mapema
akipokea Mwenge huo wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shihibu Ndemanga alisema
kuwa Mwenge huo wa Uhuru katika Manispaa ya Lindi utakimbizwa kwa urefu wa km
200 na utakagua miradi 6 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.23.
Kesho
(jumatatu, Oktoba 14) mbio hizo za mwenge wa uhuru zinatarajiwa kufikia tamati
kwa kuzimwa ambapo katika sherehe hizo za kuitimisha zitafanyika katika viwanja
vya Ilulu Manispaa ya Lindi Mkoani humo ambayo itaenda sambamba na kumbukizi ya
kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere.
No comments:
Post a Comment