Mkurugenzi wa shule ya Thobias Joachim, akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa shule ya Thobias Joachim, akimkabidhi taarifa ya shule hiyo mgeni rasmi Meneja wa benki ya CRDB Mkoa wa Pwani Rose Kazimoto.
...................................
Na Omary Mngindo, Kibamba.
SHULE
ya EMI School iliyopo Kibamba Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
inahitaji zaidi ya shilingi milioni 80 kujenga Kituo Mtaa wa Kongowe, wilaya ya
Kibaha mkoani Pwani.
Aidha
taarifa ya Mkurugenzi wa shule hiyo Thobias Joachim imetanabaisha kwamba, mbali
ya wanafunzi wanaoishi na wazazi, pia inawasomesha watoto wanaoshi kwenye
mazingira hatarishi, wanaotokea maeneo mbalimbali.
Taarifa
ya Mkurugenzi mbele ya Rose Kazimoto Meneja wa benki ya CRDB Mkoa wa Pwani
katika mahafari ya tano tangu kuanzishwa kwake, imeeleza kuwa awali walihitaji
milioni 200 kwa ajili ya kununua eneo Mtaa wa Kongowe Kibaha ili wajenge kituo
kwa ajili ya kuendeleza watoto kielimu.
"Nitumie
fursa hii kuwashukuru wazazi na walezi wa wanafunzi, pia wadau waliojitolea
katika kufanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 120 kati ya
shilingi milioni 200, tayari tumeshanunua eneo Kongowe, sasa tunatafuta fedha
kwa ajili ta kuanza ujenzi," ilieleza taarifa ya Mkurugenzi huyo.
Akizungumza
na wazazi na walezi wa wanafunzi hao, mgeni rasmi Rose alianza kumpongeza
Mkurugenzi Joachim na watumishi wake, kwa kuona umuhimu wa kuwasomesha bure
watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, huku akiwaomba wadau kujitokeza
kusaidia juhudi hizo.
"Katika
taarifa iliyosomwa na Mwalimu Mkuu imegusia changamoto ya sisi wazazi kutolipa
ada, niwaase tuwe tunalipa kwa wakati ili tusikwamishe juhudi zinazofanywa na
uongozi wa shule, pia tuache kuwahamisha watoto wetu katika shule kwa kukwepa
ada," alisema Rose.
Mwenyekiti
wa Kamati ya shule Ramadhani Sinale naye amewaasa wazazi kujitokeza katika kusaidia
maendeleo ya shule, huku akieleza kwamba imekuwa mkombozi mkubwa katika eneo
hilo kwa kuwapatia elimu safi vijana.
"Pamoja
na hayo Changamoto za uendeshaji, miundombinu, kitaaluma tunaendelea kuzitatua,
pia ada inatugusa wazazi, anajitahidi kuzitatua, hatuna vifaa vya kufundishia
kama kompyuta ambavyo ni muhimu hapa shuleni," alisema Sinale.
No comments:
Post a Comment