Na
Omary Mngindo, Chalinze.
UONGOZI
wa shule ya Sekondari ya Chalinze Islamic Modern iliyoko Kitongoji cha Chalinze
Mzee Kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, imeisaidi mifuko
10 ya saruji na rimu 15 shule ya Msingi ya Kibiki.
Shule
Kibiki iliyowahi kupatiwa cheti cha kufanya vizuri kielimu na Waziri wa Elimu
Profesa Joyce Ndalichako, iko katika hali mbaya ya kimiundombinu kutokana na
kutokuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa, matundu ya vyoo sanjali na
madawati.
Hayo
yamebainika wakati uongozi wa shule ya Chalinze Morden ulipokwenda kujitolea
nguvu kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimi,
ambapo mbali ya mifuko ya saruji pia wameshiriki uchimbaji wa msingi.
Mkurugenzi
wa Chalinze Morden Omary Swed alisema kuwa hatua hiyo wameifikia ili kuunga
mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto zinayoikabili sekta ya elimu
hapa nchini.
"Tulipata
taarifa kuhusiana na shule hii ya Kibiki yenye zaidi ya miaka kumi tangu
kuanzishwa kwake, lakini inakabiliwa na changamoto lukuki, hivyo tumeguswa na
kuja kuwaunga mkono, sio kama sisi tinacho sana, lakini tumekuja kushirikiana
na shule binafsi," alisema Swed.
Aidha
amewaomba wa-Tanzania kuendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli, na
kuendeleza juhudi anazozifanya za kuinua uchumi wa nchi, badala ya kumkatisha
tamaa.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibiki Magreth Kileo alishukuru kwa
kupata msaada huo, na kuzungumzia changamoto mbalimbali ikiwemo kutumia choo
kimoja na wanafunzi.
"Mahitaji
vyumba vya madarasa 14 yaliyopo matano upungufu tisa, wakati wanafunzi 624,
madawati 70 mahitaji 150 wapo wanaokaa katika madawati, wengine wanakaa chini,
vyoo matundu sita, kimoja cha Mwalimu vitano wanafunzi, tuna upungufu wa tundu
22," alisema Kileo.
Kwa
upande wake diwani wa Kata ya Bwilingu Lucas Lufunga amesema kuwa shule ya
Chalinze imekuwa mhimili katika ubora wa Kitaaluma kwenye Kata nzima ya
Bwilingu.
"Tunajivunia
shule hii kwani imekuwa ikitoa misaada mingi kwa jamii, mwaka huu imekuwa shule
ya 19 kwa ubora katika matokeo yaliyotolewa na serikali," alisema Lufunga.
No comments:
Post a Comment