Wananchi wametakiwa kuwa na tabia ya
kuhoji wahudumu wa afya kabla ya kuanza kutumia madawa wanayopatiwa kwenye
vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha wahudumu wa afya wametakiwa
kuwauliza maswali wagonjwa kabla ya kuwapatia vipimo ili kujua historia ya
tatizo linalomsumbua na kutoa dawa sahihi.
Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri
wa afya Jinsia Wazee na Watoto Dr.Faustine Ndugulile akiwa katika ziara ya
kikazi mkoani Manyara ambapo amesema, wananchi wananyweshwa madawa mengi ambayo
hayana msingi hali inayowasababishia kupata matatizo mengine ya kiafya.
Amesema kitaalamu asilimia zaidi ya
themanini 80% ya Homa ambazo watanzania wanaugua si malaria,Typhod wala U.T.I,
bali homa nyingi zinasababishwa na virusi ambayo havina tiba isipokuwa ni
ugonjwa ataokaupata baada ya siku tatu hadi wiki moja mgonjwa anapata nafuu.
Naibu Waziri Dr. Ndugulie alisema
Vipimo vya magonjwa ya UTI na Typhod havipimwi kwa dakika 10 au saa kama
inavyofanyika kwa sasa bali ni mchakato wa zaidi ya masaa 48 hadi 72 ndipo
vimelea vya ugonjwa huo viweze kuonekana.
“Mwananchi ukienda kwenye kituo cha
kutolea huduma ya afya na ndani ya dakika 15 ukaambiwa unagua UTI au
Typhod muulize daktari maswali ya msingi,wewe umweza kumebaini ugonjwa huu kwa
kutumia njia gani?”alisisitiza Dr.Ndugulile
Dr.Ndugulile amesema kinachofanywa
katika vituo vya kutolea huduma ya afya ni Biashara na sio kumtibu mgonjwa kwa
dawa inayoendana na ugonjwa unaosibu.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii jinsia wazee na watoto Dr. Faustine Ndugulile ametembelea hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Manyara kukagua shughuli mbali mbali ambazo
zinatekelezwa chini ya wizara ya afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia wazee na watoto
kupitia idara zake kuu mbili za Afya pamoja na Maendeleo ya jamii.
Amesema wizara ya Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia wazee na watoto inaendelea kujipanga kuhakikisha huduma katika
hospitali za rufaa za mkoa zinaboreshwa na kuendelezwa ambapo katika bajeti ya
mwaka 2018/2019 serikali imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya kuimarisha
hospitali za rufaa zilizopo na kujenga nyingine mbili mpya katika mkoa wa
Simiyu na Njombe ambapo maeneo yatakayopewa kipa umbele katika hospitali
hizo ni huduma ya magonjwa ya dharura,chumba cha wagonjwa mahututi kwa watoto
na watu wazima,kuimarisha huduma ya mama na mtoto.
Pamoja na yote hayo Dr.Ndugulile
amwaleza watanzania kuwa serikali imeendelea kupambana na ugonjwa Malaria mabo
hadi kufikia sasas mwaka 2018 ugonjwa huo umepungua toka asilimia 14%
Miaka miwili iliyopita hadi kufikia asilimia 7%
No comments:
Post a Comment