Afisa
Ushirikishaji Wanaume wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Bw. Kiswigo Ibrahim
Mwan`gonda akiongea na washiriki kuhusu
dhumuni la kongamano hilo mapema jana jijini Dar es salaam.
Imeelezwa kuwa wanaume wanawajibu wakumtetea mtoto wa
kike dhidi ya vitendo vya kikatili vina mzunguka, hiyo ni kutokana na ukweli kuwa wana uwezo wa kukataa vitendo hivyo kwakupaza sauti zao lakini
pia kukataa kutoa ruhusa kwawamama wanaojishughulisha navitendo vyakikatili.
Akizungumza katika
bonanza maalum la michezo lenye dhamira yakutoa elimu kwa wanaume, Afisa Ushirikishaji Wanaume wa Jukwaa
la Utu wa Mtoto (CDF) Bw. Kiswigo Ibrahim Mwang'onda amesema wanaume wakiamua wanaweza.
Bw. Mwang’onda amesema kwamuda mrefu mapambano yakumtetea mtoto wa kike
dhidi ya ukatili vilikuwa vinahusisha wanawake wenyewe sasa wameamua kutoa elimu hiyo kwa wanaume ili nao waweze kusaidia kumlinda mtoto wa
kike.
Lengo
la bonanza hili ni kuwakutanisha na kuwaunganisha wanaume kupitia michezo na kuwahakikisha wanaume wanapata ujumbe kuwa wao wanajukumu kubwa
la kuhakikisha wanalinda na kuthamini haki za mtoto wa kike.” Aliongeza Mwang’onda.
Aliendelea kusema kwakuwa wanaume ni sehemu kubwa ya tatizo
la ukatili wa kijinsia na ndio watekelezaji wakubwa wa ukatili huo wameamua kukaa nao ili kutafuta suruhisho
la
kudumu kuhusiana na tatizo hilo ili kuhakikisha watoto wa kike wanaishi katika jamii yenye haki na usawa.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi katika bonanza hilo, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Bi. Joyce Maketa amesema hali ya ukatili kwa watoto wa kike
imeendelea kupungua katika wilaya ya Ilala sababu ikitajwa kuwa nimipango thabiti iliyowekwa na Serikali ya awamu ya tano Chini ya Jemedari Rais
John Pombe Magufuli.
Aidha afisa huyo alisema kuwa amefurahishwa na
bonanza hilo lililoandaliwa na CDF pamoja na ISDI kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Uswidi (SIDA)
kwa kuweza kuwakutanisha vijana wa kiume nawanaume ili wawe mabalozi wazuri wakutetea nakupigania haki za mtoto wa
kike ambazo atazipoteza kama hatopewa ulinzi stahiki na jamii inayomzunguka.
Afisa
Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Joyce Maketa(kushoto) akifuatilia kwa karibu
bonanza, (katikati) CDF kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
ISDI Bw. Jonas Tiboroha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la ISDI Bw. Jonas Tiboroha akielezea kwa ufupi shughuli
zinazofanywa na shirika hilo.
No comments:
Post a Comment