Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika
mashariki Balozi Agustine Mahiga akitoa hotuba kabla ya kuyafungua maonyesho
hayo ya siku moja mwishoni mwa wiki jijini arusha picha na mahamoud ahmad
arusha.
............................
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki na Kikanda, Dk, Agustine Mahige amesema kuwa Tanzania
haijamfukuza balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Reoland van de Geer bali
ameitwa nyumbani na Umoja wa nchi hizo kw mshauriano.
Aidha amepongeza mashirika ya
Kimataifa yaliyopo nchini kwa kuandaa siku maalum ya kuwaonyesha wananchi fursa
na kazi wanayofanya katika kukuza uchumi ikiwemo kuhakikisha muuaji ya kimbari
yaliyotokea nchini Rwanda hayajirudii tena.
Akizungumza Leo Novemba 3,
Jijini Arusha katika maonyesho ya mashirika ya kitaifa yenye
makao makuu yake Jijini Arusha Dk, Mahige alisema kuwa ni jambo la
kawaida kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao kuitwa na nchi zao kwaajili ya
kupewa majukumu mengine au kutoa tathimini ya masuala waliyoyafanya.
Dk, Mahige alisema uwepo wa Mahakama
inayoshugulikia muuaji ya kimbari (MICT) ni kuhakikisha muuaji ya kimbari
hayatokei tena katika nchi za Afrika na kutoa rai kwa mashirika ya Kimataifa
yaliyopo nchini kutunza kumbukumbu muhimu ikiwemo za muuaji ya kimbari.
Alisema maneno au vitendo
yanayotolewa na wananchi katika nchi mbalimbali yanatakiwa kupingwa kwa nguvu
zote kwani yanaweza kuibua hisia na kupeleka muuaji au kuleta chuki baina ya
watu na watu au hata kupeleka mauaji.
Alisisitiza kuwa ni vyema sasa
mahakama hiyo ikawajengea uwezo wanazuoni wa masuala ya kisheria kwa Tanzania
na nchi za Afrika ikiwemo kuzingatia utawala wa sheria na demokrasia pamoja na
haki za binadamu.
Awali Mkuu wa shughuli za Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez alisema kuwa Tanzania inajitahidi
kukahakikisha malengo endelevu yanazingatiwa ikiwemo kuhakikisha maendeleo
yanapatikana kwa kila mtanzania.
Naye Afisa Mwandamizi wa Utafiti
kutoka Taasisi ya Sheria za Kimataifa, Profesa Mathias Sahinkuye alisema
masuala ya sheria ni muhimu ili kuhakikisha nchi zinakuwa na amani
Awali Meya wa Jiji la Arusha Kalist
Lazaro,ambaye ndiye mwasisi wa Maonyesho hayo amesema tangu kuanza kwa
Maonyesho hayo mwaka Jana kumekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii kujifunza
fursa mbalimbali za Kimataifa.
“Mjumuiko wa wananchi katika
Maonyesho hayo ya Kimataifay umekuwa na manufaa makubwa kwani kumekuwepo na
mabadiliko na mafanikio makubwa kwa wananchi kujifunza na kujionea fursa za
kibiashara” Amesema Meya.
No comments:
Post a Comment