Friday, November 30, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 20 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA.NOVEMBA 30,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018(PICHA NA IKULU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018

MALALAMIKO 74 UKATILI WA KIJINSIA YARIPOTIWA LINDI.

NA HADIJA OMARY, LINDI

Jumla ya Malalamiko (74) yanayohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani humo,yamefikishwa katika Dawati sheria ,huku vitendo vya ubakaji vikiwa vinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa,mwaka 2017

Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Anna Maro alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG  Ofisini kwake mjini humo, kuhusiana na siku (16) kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika manispaa hiyo

Maro alisema vitendo hivyo vimeripotiwa kituo cha Polisi cha Lindi mjini,kupitia Dawati lake la kijinsia, na kwamba wamefanyiwa ukatili huo,kipindi cha mwaka mmoja uliopita,kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2017.

Alieleza kwamba vitendo vya ubakaji ndio unaoongoza kwa kuwa na Idadi kubwa (39),ikifuatiwa kujeruhi na Shambulio la mwili,iliyo na idadi (9) kila moja,Mimba za wanafunzi (7),kulawiti (3),wakati kutelekeza familia na matumizi ya Lugha za matusi zikishika mkia kwa kuwa na idadi ya moja kila moja.

Maro alisema katika malalamiko hayo,yaliyofikishwa Mahakamani na kutolewa uwamuzi ni kesi tatu zinazohusu ukatili dhidi ya kulawiti, ambapo wahusika wamepewa adhabu ya kutumikia Gerezani kifungo cha maisha.

Pia,alisema anashangazwa na matumizi ya Lugha ya matusi inavyoendelea kutumika na Jamii,lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika .

Hata hivyo maro ametaja mikakati ya kupunguza tatizo hilo ni pamoja na kutumia kamati ya Mtakuwa kufanya kazi ya kuelimisha Jamii kuanzia ngazi za Mitaa,Kata na Halmashauri mzima ya Manispaa ya Lindi.

BABA MZAZI AUWA WATOTO WAKE WATATU BAGAMOYO.

Kamanda wa polisi wa mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo . (picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………….
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi ,waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao mzazi.

Chanzo cha kutenda kitendo hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa watoto hao.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

Aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji cha Kunwe ,Mvomero mkoa wa Morogoro .

Wankyo alibainisha,baba wa watoto hao alikuwa na mgogoro na mkewe ambae ndiye mama wa watoto .

“Mtuhumiwa alipowafuata watoto kutoka kwa mama mkwe wake kwa madai kwamba anakwenda kucheza nao na angewarudisha baadae ” alifafanua Wankyo.

Alielezea,mtuhumiwa aliwapakia marehemu kwenye baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele ,Kibindu ambapo aliwanywesha dawa hiyo kwa kuwachanganyia na juisi hivyo kupelekea vifo vya watoto hao.

Kamanda huyo alisema ,katika eneo la tukio kumeokotwa chupa mbili za juisi zilizotumika ,chupa ya dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

“Mara baada ya tukio mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa matibabu” Wankyo aliweka bayana.

Mpaka sasa hali yake sio nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi wa polisi .

Katika hatua nyingine ,Wankyo alisema jeshi hilo limekamata viroba saba vya bangi vilivyokuwa vikisafirishwa kwenye gari yenye chesesi namba V75w – aina ya mitsubishi station wagon huko Kijiji cha Mwatemo kata ya Kiwangwa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo. 

Thursday, November 29, 2018

MAKUSANYO HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAONGEZEKA.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa  (kushoto) na Makamo Mwenyekiti Halmashauri hiyo (kulia) Saidi Ngatipula.
.....................................

 Halmashauri ya Bagamoyo, mkoani Pwani ,imekusanya zaidi ya sh. bilioni 2.313 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mapato ya mwezi ya sh. bilioni 2.727.6 kwa kipindi cha mwezi septemba mwaka huu. 

Makusanyo hayo yanafanya jumla ya makusanyo kutoka mwezi julai hadi septemba kuwa bilioni 6.692.611.969 ambayo ni sawa na asilimia 20 ya makusanyo yaliyokisiwa kukusanywa kwa mwaka. 

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ally Ally Issa wakati akitoa taarifa ya fedha ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwezi septemba, ikiwa ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Aidha Issa alisema, halmashauri hiyo kwa mwezi septemba imekusanya milioni 159.085.524 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani. 

Hata hivyo mwenyekiti huyo ambae pia ni diwani wa kata ya Fukayosi alisema, mapato ya septemba yameongezeka ukilinganisha na mapato ya mwezi agost mwaka 2018.
Issa alisema, kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 ilikisia kutumia bilioni 32.371.697.034 .

“Kiasi cha 368.958.970 zilivuka mwaka wa fedha 2017/2018 ,kiasi hicho kitakuwa ni sehemu ya matumizi kwa kipindi cha 2018/2019 hivyo kufanya jumla ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuwa bilioni 33.100.926.004”

Akizungumzia mikakati waliyonayo katika kipindi cha 2018/2019 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa alisema ni kuhakikisha kwamba wanasimamia mapato na matumizi ili kulenda maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Alisema kwa sasa Halmashauri hiyo imejipanga kuboresha vyanzo vya mapato ili kuongeza kasi ya ukusanyaji.

Aidha, aliongeza kuwa, tayari Halmashauri imeshapata eneo litakalojengwa kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani na kwamba kituo itakuwa ni sehemu ya kukusanyia mapato.

Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo wakiwa katika kikao cha Baraza
 
Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo wakiwa katika kikao cha Baraza

NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU ZIARANI MKOANI IRINGA.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe ikiwa ni kuashiria uwashwaji wa umeme katika kijiji cha Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini.
 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akibonyesha kitufe cha kuwashita taa na kingora ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa kazi ya kuwasha umeme katika kijiji cha Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini. Kijiji cha Igula ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi wa kupeleka kwenye vijiji vilivyopitiwa na Njia kuu ya Umeme KV 400.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwasha umeme katika kijiji cha Igula iliyopo halmashauri ya Iringa Vijijini. Kutoka kushoto ni Katibu tawala, Hashimu Komba na Diwani wa Kata ya Kihologota, Paziyano Kayage.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi Ikengeza iliyopo halmashauri ya Iringa vijijini. Shule hiyo ni miongoni mwa taasisi ambazo zimenufaika na mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vilivyopitiwa na Njia kuu ya Umeme ya KV 400(BTIP-VEI).
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akimbana msimamizi wa Kampuni ya Sengerema Engineering Group, Bryson Chengula baada ya kutolidhishwa na kazi ya utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ambao unatarajia kufikia tamati Juni 30 mwakani.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 29, 2018.

Wednesday, November 28, 2018

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA PALESTINA PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuonyesha viungo vya chai kutoka Zanzibar Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) wakati wa kumkabidhi kama zawadi, Mheshimiwa Balozi wa Japan alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)

KATIBU MKUU NYAMHANGA AKAGUA DARAJA LA KAVUUU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, kuhusu kuifanyia matengenezo barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130 kwa kiwango cha changarawe, mkoani humo.
 
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu ukamilikaji wa Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani humo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoka kukagua kingo za Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limekamilika na limeanza kutumika kwa magari yasiozidi tani 30.
Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa mita 85.344linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.718.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano