SHEIKH RAMADHANI MOHAMED WA TANGA AFARIKI DUNIA.

Image may contain: one or more people and text
Mudir Idara ya Daawah Markaz kuu Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Sheikh Ramadhan Muhammad (Bonge) amefariki dunia usiku wa saa tisa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.

Taarifa kutoka nyumbani kwao zinasema muda wa saa saba za usiku alipatwa na pressure ya ghafla hali iliyopelekea kuwahishwa hospitalini na hatimae kufariki dunia Jumatatu ya leo ya tarehe 29.07.2019 mil.

Huyu ndiye aliyekuwa muhimili mkubwa wa Daawah katika Idara hiyo ndani ya Taasisi ambapo Muhaadhara wa mwisho katika uhai wake ameufanya jumapili katika ukumbi wa Asmaa bint Abubakr Asw-swiddiq (Radhwiyallaahu 'anhaa) siku ya jumapili iliyopita.

Naibu Mudir Markaz kuu Sheikh Ally Nassor (Hafidhwahullaah) anatoa pole za Taasisi kwa ndugu na jamaa na umma kwa ujumla na wanasunna hasa kwani alikuwa mmoja viongozi shupavu ktk swafu yetu mpaka anafariki.

“Ee Allaah, Msamehe na Umrehemu na Umuafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Upanue kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).

Taarifa za mazishi zitatangazwa Inshaa Allaah.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA UTANGAZAJI MARKAZ KUU.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AUNGURUMA PWANI ASEMA DHAMIRA KUBWA YA CCM NI KUWAHUDUMIA WANANCHI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016 HAYA HAPA

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA