Posts

Showing posts from November, 2026
Image
WANANCHI ELFU 30 MANISPAA YA KIBAHA WAPATA NEEMA KUBWA  YA MSAADA WA KISHERIA  Na Victor Masangu,Kibaha  ZAIDI ya wananchi wapatao  elfu 30 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani  wamefanikiwa kupatiwa  huduma za msaada wa kisheria bure kupitia  Kampeni  ya  Mama  Samia  awamu ya pili na kupata fursa ya kusaidiwa mambo mbali mbali yakiwemo utatuzi  wa migogoro mbali mbali ikiwemo ardhi,ndoa, ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake   pamoja na kupatiwa ushauri na elimu ya masuala ya kisheria   Hayo yamebainishwa na Wakiri wa serikali kutoka Wizara ya katiba na sheria Kasilida Chimagi wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na mwenendo mzima kuhusiana  na  zoezi la kampeni hiyo  ambapo amebainisha kwamba wananchi wengi wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuweza kupatiwa huduma hiyo. Amesema kwamba katika zoezi hilo la kuwasikiliza wananchi wameweza ku...

RC MABULA ATAKA KASI MPYA YA MAENDELEO TABORA

Image
 RC MABULA ATAKA KASI MPYA YA MAENDELEO TABORA Na Allan Kitwe, Tabora MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt Angeline Mabula amepokelewa rasmi katika Mkoa huo na kueleza wazi kuwa anataka kuona Mkoa huo ukipiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo na kila mtumishi kutimiza wajibu wake ipasavyo. Ameeleza hayo jana alipokuwa akiongea na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi, Sekretarieti ya Mkoa, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Maafisa Tarafa. Amesema kuwa Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa yenye fursa nyingi za kiuchumi, lakini utekelezaji wake hauridhishi licha ya jitihada zinazofanyika, hivyo akasisitiza kuwa anataka kuona Tabora ikienda kwa kasi zaidi. Ametaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni maeneo ya uwekezaji viwanda, bwawa la Wembele, eneo la ujenzi wa Bandari Kavu, Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo unaoendelea sasa na nyinginezo. ‘Najua baadhi ya mipango utekelezaji unaendelea, ila kasi yake hairidhishi, na hili ndilo nalotaka lifanyik...