ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi
(UWT) Wilaya ya Ilala Norah Waziri (52), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kinondoni kwa shtaka la kughushi cheti
cha ndoa.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Benson Mwaitenda,
akimsomea shtaka lake mbele ya Hakimu, Anifa Mwingira, alidai Februari 4 mwaka
1995 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya
kudanganya mtuhumiwa alighushi cheti cha ndoa chenye namba za usajili
00040078 kikionyesha ameolewa na
Silvanus Mzeru katika Kanisa Katoliki la Mburahati.
Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo mwendesha mashitaka
alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Hakimu Mwingira alisema dhamana ipo wazi kwa mashariti
ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua zinazo watambulisha
wanapotokea, vitambulisho vya Taifa na kusaini bondi ya Sh milioni moja.
Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza
mashariti na kesi hiyo itatajwa tena Julai 17.
Wakati huo huo watu wawili amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la mauaji.
Waliofikishwa Mahakamani ni Juma Malumbi (34) mkazi wa
Kinondoni Hananasif na Amri Mazangu (40) mkazi wa Mbagala Kirulugwa.
akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, ASP Hamisi, alidai Octoba 20 mwaka 2018 maeneo ya Bonde la
Mchicha Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, watuhumiwa walimuua Zurufa
Oda.
Hakimu Mushi alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu
chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
ASP Hamisi alidai upelelezi hauja kamilika na kuomba
tarehe nyingine kwa kesi hiyo kutajwa
No comments:
Post a Comment