Muonekano wa Gari aina ya Haice
yenye Namba za usajili T239 DMA, baada ya kupata ajali katika Mtaa
wa Mto Mkavu ,kata ya Mbanja Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo ikiwa
inatokea Kijiji cha Kiranjeranje wilayani kilwa ikielekea Mjini Lindi.
...................................
NA
HADIJA HASSAN 04/07/2019 LINDI
Watu
Wanne (4) wamefariki Dunia na wengine 10 kujeruiwa baada ya Gari aina ya Haice
yenye Namba za usajili T239 DMA kugonga kwa nyuma Tela lenye namba za usajili T747
DKA la Lori lenye Namba za usajili T176 DKA Mali ya Kampuni ya Saruji ya
Dangote.
Ajali
hiyo imetokea majila ya saa moja na nusu usiku wa Tarehe 02/07/2019 katika Mtaa
wa Mto Mkavu ,kata ya Mbanja Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo ikiwa
inatokea Kijiji cha Kiranjeranje wilayani kilwa ikielekea Mjini Lindi.
Gari
hiyo inamilikiwa na mohamedi juma hamisi mkazi wa Manispaa ya Lindi na inafanya
safari zake katika Manispaa hiyo na kwenda kiranjeranje wilayani kilwa Mkoani
humo.
Nae
Abdurahman Shabani Mwenyekiti wa Mtaa wa Mto Mkavu alisema kuwa kabla ya Ajali
hiyo kutokea Dereva wa Gali ya Dangote alisimamisha Gari yake pembezoni mwa
Barabara ambapo inasadikika alikuwa anafanya marekebisho ya Gari yake ndipo
Gari hiyo ya Haice ikaenda kuligonga lori hilo kwa nyuma.
“kabla
ya ajali kutokea Yule Dereva wa Dangote alipaki Gari yake kwa ajili ya kufanya
marekebisho madogo ndipo Haice ile ikaja kugonga kwa nyuma kwa pembeni baadae
ikayumba na kuangukia kichakani ambapo licha ya kugonga lakini pia ilikanyaga
miguu ya Dereva wa Dagote ambae alikuwa chini ya Gari yake akifanya marekebisho
hayo” alisema Shabani.
BAGAMOYO
KWANZA BLOG ilifika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine ambapo
ilikutana na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Jumanne Shija, ambapo
alithibitisha kupokea majeruhi kumi(10) na miili ya Marehemu wanne(4) wa ajali
ya Gari siku ya jumanne majira ya saa mbili na nusu usiku.
Alisema
kati ya majeruhi hao kumi waliowapokea Mmoja akiwa ni mtoto wa kike, wawili
waliwatibu na kuwaruhusu kurudi majumbani kwao, sita walibaki hospitalini kwa
ajili ya kuendelea na matibabu na wawili kulingana na majeraha waliyonayo
walilazimika kuwapa rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kupatiwa matibabu zaidi Kuhusu miili ya Marehemu waliowapokea katika Hospitali
hiyo.
Shija,
alisma Madaktari wameshaifanyia uchunguzi pamoja na kuwatambua Marehemu hao
ambapo wanawasubiri Ndugu wa marehemu kwa ajili ya kuwachukuwa.
Nao
Baadhi ya majeruhi waliokuwa katika Ajali hiyo akiwemo Robson Moleli na Selemani
Sabiini walidai kuwa chazo kikubwa cha kutokea kwa Ajali hiyo ni mwendo mkali
wa Gali hiyo ya Haice ambayo ilikuwa inakimbizana na Gari nyingine aina ya
costar hali ambayo Dereva wa gali hiyo alishindwa Kuchukuwa tahadhari ya haraka
ya kuliweka sawa gari yake mara moja baada ya kuliona Lori lililokuwa limesimama
mbele yake.
Sabiini
alisema kwa Madereva wa Magari Madogo kwenda mwendo wa kasi na kukimbizana ni
kawaida yao , mara nyingi wanadai kuwa wanakimbilia Abiria katika vituo vya
Magari vinavyofuata lakini cha ajabu kwa siku hiyo ya jana hakukuwa na shida ya
abilia maana magali yote yalipata abiria mpaka wengine waliwaacha kwa kushindwa
kuwabebe katika stendi ya Mchinga” alisema.
“Ila
kikubwa baadhi ya madereva hawa wanapenda ushindani usio na maana wanakuwa na
michezo ya kupima uwezo wa gari kutembea bila kujua kwamba wamebeba dhamana za
Roho za watu katika magari yao” aliongeza.
Nae
moleri alisema kuwa kutokea kwa ajali hiyo kumeathiri kwa kiasi kikubwa katika
shuguli zake za kiuchumi kwani kutokana na kulazwa Hospitalini hapo atashindwa
kufanya biashara zake za kila siku.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Pudensiana Protas
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha Ajali hiyo ni
Dereva wa Haice kushindwa kuchukuwa Tahadhari baada ya kulikuta roli na baadae
kuligonga kwa nyuma hali iliyosababisha vifo na majeruhi kwa abiria waliokuwepo
kwenye gali hiyo.
Kamanda
Protas pia aliyataja majina ya Marehemu katika Ajali hiyo kuwa ni Hasani Omary
(45) Msambaa mkazi wa Dar es salaam, Abdallah Musa Ngalawa (25) Mmakonde
Kondakta wa Haice hiyo Mkazi wa Lindi Mjini, Muhibu Abdallah (Kampunda) Mkazi
wa Kariakoo Lindi Samweli Warioba Mkazi wa Mpilipili Lindi.
Hata
hivyo Kamanda Protas aliwataja Majeruhi wa Ajali hiyo kuwa ni Selemani Saidi (
67) Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Mambo (36) Dereva wa Gari ya Dangote
mzigua mkazi wa Dar es salaam, Mwanaidi Hassani (5) Mkazi wa Ng’apa Lindi,
Robson Moleri (25) Mmasai Mkazi wa Kariakoo Lindi.
Wengine
ni Ally Isumail (41) Mndengeleko Mkazi wa Lindi Majeruhi wengine ni Shufaa
Bakari(21) Mwera Mkazi wa Ng’pa Lindi, Angetus Kajuni (20) Mnyakyusa Mkazi wa
Manspaa ya Lindi, Saidi Saidi (30) Mkazi wa Manispaa ya Lindi, Yusuph Saidi(36)
Mmwela Mkazi wa Lindi, Azizi Tehabu(41)
Majeruhiwa ajali hiyo wakipata huduma ya matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Muonekano wa Gari aina ya Haice
yenye Namba za usajili T239 DMA, baada ya kupata ajali katika Mtaa
wa Mto Mkavu ,kata ya Mbanja Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo ikiwa
inatokea Kijiji cha Kiranjeranje wilayani kilwa ikielekea Mjini Lindi.
Wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakitoa matibabu kwa majeruhi.
Askari wa usalama barabarani mkoani Lind, akiwajibika kupima eneo lililotokea ajali.
No comments:
Post a Comment