Waziri wa viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya Wanachama wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) wakizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa viwanda na
Biashara Innocent Bashungwa ameonyesha kusikitishwa kwake na adha wanayoipata
wajasilimali wadogo pamoja na vijana ya kukosa vifungashio vyenye bei nafuu na
kwa haraka, jambo lilomsukuma kuamua kukutana na shirikisho la wenye viwanda Tanzania
(CTI) kujadili mikakati ya kulimaliza changamoto hiyo.
Akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kuzungumza na shirikisho la wenye viwanda Tanzania, Bashungwa
amesema wakina mama, vijana na wajasiliamali kwa ujumla wake wanakubwa na
changamoto ya vifungashio vya bidhaa zao wanazozisindika, sababu kubwa ikiwa ni
bei lakini pia wengi wao wana mtaji mdogo na hawawezi kununua vifungashio kwa
wingi.
“Wengi wa wajasiliamali wanauwezo
mdogo wa kuagiza vifungashio kwa mkupuo,
kupitia CTI muunde chama ambacho kitaweza kuwasaidia wazalishaji wadogowadogo
kupata vifungashio. Ni fursa kubwa kama ikitumiwa vizuri, kwa sababu kuna
changamoto ambayo inahitaji majibu.
Katika hatua nyingine
amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inawahakikishia wamiliki
wa Viwanda nchini kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayoimarisha
ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuweka mipango mahususi ya kuongeza
uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya Masoko katika nchi za Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC).
Amesema Serikali na wamiliki wa Viwanda kunatakiwa kuwe na ushirikiano wa karibu ili kutatua changamoto ambazo viwanda inakabiliana nazo, ikiwemo changamoto za nje ya mipaka ya Tanzania.
“Nimesikia changamoto
nyingi hapa kutoka kwenu ndugu zangu wa CTI, zipo zinazohitaji sera, sharia kufanyiwa
marekebisho, lakini pia zipo ambazo za muda mfupi, nataka kuwaambia hapa
tutafanya kila liwezekanalo kutatua changamoto hizo ili muweze kukua kwenye
uzalishaji,” alisema
Alisema lengo la serikali
ni kuona viwanda vya Tanzania vinakuwa na soko kubwa ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania, huko tutafika kama tukiwa na umoja
Amesema Takwimu
zinaonyesha kuwa viwanda vya ndani vinazalisha chini ya uwezo wao, jambo ambalo
ni hasara kubwa na halikubaliki.
“Kaka Tenga
utanisahihisha hapa, naambiwa uzalishaji wa viwanda vyetu vya ndani ni chini
asilimia 30% tu, aslimia zingine 70% zimekuwa zikipotea bure, yaani ni hasara,
tushirikiane tuone kwa nini hatuwezi kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa,”
alisema
Amesema Tanzania inapaswa
kutumia fursa ya masoko ya nchi wanachama ikiwamo SADC, na Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Akifafanua amesema kuwa
sekta ya Viwanda inasaidia kuzalisha ajira na kuchangia katika kuwezesha
maendeleo endelevu kwa kuimarisha viwanda vilivyopo na vipya kwa maendeleo ya
nchi yetu.
Akizungumzia changamoto za sekta hiyo Mhe Bashungwa amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuchukua changamoto za wamiliki wa Viwanda na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka ili dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda itimie kwa wakati kwa maslahi mapana ya Taifa na wamiliki wa viwanda hivyo.
“Serikali ya Awamu ya Tano na Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli inatoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa dhana ya ujenzi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo kwa kujenga mazingira wezeshi katika sekta hii muhimu kwa ujenzi wa viwanda” Alisisitiza Mhe. Bashungwa.
Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Bashungwa umelenga kuimarisha sekta ya viwanda hapa nchini kwa kuweka mikakakati itakayowawezesha kumudu ushindani wa bidhaa kutoka nje.
Aidha Bashungwa ametumia
fursa ya mkutano huo kuwashauri shirikisho la wenye viwanda Nchini kutumia
fursa ya mkutano wa SADC kuangalia namna watakavyoweza kushirikiana na wenzao
ili kuongeza wigo wao wa biashara.
Ends.
No comments:
Post a Comment