Na Selemani Magali; Daresalaam
WAKALA wa misitu Tanzania (TFS) imewataka watanzania
kutembelea vivutio halisi ili kujionea utajili uliopo hapa nchini.
Imesema idadi ya watanzania waotembelea vivutuo vya asili
ni mdogo licha ya kuwa wanalipia Sh2,000 pekee kama kiingilio katika maeneo
hayo huku wageni wakilipa Dola 10 za kimarekani.
Kutokana na
hilo Mamlaka ya misitu Tanzania (TFS) imeandaa safari ya siku tatu kwa ajili
Wananchi watakaopenda kutembelea msitu wa Magamba uliopo katika eneo la Lushoto
Mkoani Tanga.
Akizungumza
katika maonyesho ya sabasaba wakati Naibu waziri wa Maliasili na utalii
alipotembelea maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa, ofisa utalii na Mafunzo, Samiji Mlemba
amesema safari hiyo ipo na wangependa kuona wananchi wanajitokeza kwa wingi
kwenda kuona msitu wao uliopo hapo Tanga.
Mlemba alisema watanzania wengi wamekuwa
wakishindwa kujua umuhimu wa kutembelea vitu vya asili na kujifunza ili kuweza
kuongeza kitu kipya.
“Katika mwaka wa fedha ulioisha tulipokea watalii
zaidi ya 3,000 na kati yake 594 pekee ndiyo walikuwa kutoka nchini na mara
nyingi huonekana katika msimu wa sikukuu ya pasaka na Mwisho wa mwaka.” Alisema
Mlemba
Alisema katika safari ya siku tatu waliyo iandaa
wamejipanga kuhakikisha kuwa idadi ya watanzania wanaokwenda inakuwa kubwa ili
waweze kujifunza na kutambua vivutio vilivyopo nchini.
“Katika eneo hilo kuna mahandaki ya vita ya kwanza
ya dunia, maporomomo ya maji, nyumba za asili, shughuli mbalimbali
zinazoendelea na ili kushiriki safari hii mtu mzima atalipia Sh171,000 na mtoto
Sh148,000 ikijumuisha malazi, chakula na usafiri.” Alisema
No comments:
Post a Comment