Friday, July 5, 2019

WAFANYAKAZI WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA WCF SABASABA ILI KUPATA ELIMU NA KUJUA HAKI ZA MFANYAKAZI NA MWAJIRI


Mkurugenzi wa Huduma na Tathimini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF),Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema mfanyakazi aliyeumia kutokana na kazi aifanyayo au maradhi yaliyosababishwa na kazi ifanyayo.
Mfuko utagharimia matibabu kwa ujumla baada ya kufanyiwa tathmini na madaktari ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya tathmini kwa Mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi kutokana na kazi anayoifanya.
Naye Mkuu wa kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa (WCF),Bi. Laura Kunenge, aliwahimiza waajiri na wafanyakazi kutembelea banda hilo ili kupata elimu lakini pia kujua haki za mfanyakazi na mwajiri.
“Mfulo huu unatoa nafuu sio tu unasaidia Mfanyakazi kulipwa Fidia Stahili bali pia unatoa nafuu kwa mwajiri kwani ghara hizo zitasimamiwa na WCF na sio Mwajiri. “Ndio maana tunawahizimiza waajiri kote nchini kutoka sekta binafsi na umma, kutoa michango ya kila mwezi kama sheria inavyotaka.”Amesema Bi. Laura.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF katika  banda la mfuko huo  kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa leo Dar es Salaam 2019, barabara ya Kilwa.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD),Bi. Laura Kunenge akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba  wananchi wafike katika banda la mfuko huo ili kujua haki za mfanyakazi na mwajiri kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam 2019.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgencealie (wapili kulia) akiwapatia maelezo waandishi wa habari (kushoto) kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.

Watumishi wa WCF (kulia) wakiwahudumia mwananchi waliofika kwenye kwenye banda            hilo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam2019.

No comments:

Post a Comment