WALIOSAMBAZA PICHA ZA WANAWAKE MTANDAONI KUSHTAKIWA


Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga

Mtandao wa kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesikitishwa na vitendo vya kusambazwa kwa picha zinazoonesha wanawake wanne, katika mitandao ya kijamii waliokuwa wakituhumiwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi cha Mburahati Jijini Dar es Salaama kwa makosa ya jinai.

Akitoa tamko kwa niaba ya mtandao huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga, amesema vitendo hivyo ni vya udhalilishaji wa utu wa mwanamke, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuingilia uhuru wa faragha.

"Katika hali isiyokuwa ya kawaida picha za wanawake hao zilisambaa mitandaoni na imethibitika kwamba zilipigwa na maofisa wa polisi wa kituo cha Mburahati na tuliongea na Mkuu wa kituo hicho na akathibitisha kwa kusema zilipigwa kwa manufaa ya kikazi lakini tukaziona kwenye mitandao'' Amesema Anna Henga.

Aidha mtandao huo umetoa wito kwa Jeshi la polisi, kuwachukulia hatua za kinidhamu wahusika wa kitendo hicho ili kulinda utu wa mwanamke na watuhumiwa wa makosa ya jinai.

Ameongeza kwamba mtandao huo hautosita kuchukua sheria, ikiwemo kufungua mashtaka kwa wahusika wa tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.