Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Peter Maduki akizungumza na waandishi wa habari |
Na Selemani Magali; Daresalaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi (VETA), Peter Maduki ameutaka uongozi wa VETA
kuhakikisha wanafikisha ubunifu unaonyeshwa katika maonyesho ya sabasaba
vijijini.
Maduki amesema faida ya ubunifu huo utaonekana kama wadau
watanufaika nao, ubunifu huo ukipelekwa vijijini utawasaidia sana wakulima.
Amesema wakulima
wanachangamoto nyingi ili kufikia malengo yao ikiwemo kukosekana kwa mashine za
kuchakata mazao yao, na Veta imekuwa ikionyesha mashine za kujibu changamoto za
wakulima sasa ni wakati wa kupeleka huduma hiyo Mikoani.
“Tunataka malighafi ambazo zimeshachakatwa ili kusudi zipate
thamani zaid, ukichakata unapata bei ya juu ukilinganisha na mali ghafi, ni
vema twende huko tukawasaidie wananchi.
Aidha Mwenyekiti huyo hakusita kuonyesha furaha yake kuona
vijana wanaweza kutumia kile walichojifunza darasani, hiyo ni hatua kubwa
ambayo inatia moyo kwa mzazi na taifa kwa ujumla.
Pia amefurahishwa baada ya kuona VETA sasa inaweza kutoa mchango
katika kuchangia kuimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa Tanznia hasa eneo
la usindikaji wa mazao ya Kilimo kwa ajili ya viwanda viwanda vya ndani.
Mwenyekiti anasema tayari serikali imeshawawezesha VETA kubuni
miradi mbalimbali sasa ni zamu ya mamlaka kuhakikisha inasaidia wakulima
kuongeza thamani ya mazao yao na wanufaike na ubunifu wa VETA.
Aidha amesema VETA wanashirikiana na Shirika la kuendeleza
Viwanda vidogo vidogo (SIDO) pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
ili kuweza kufikia lengo la uchumi wa viwanda waliojiwekea watanzania kwa
kushirikiana na Serikali.
“Kwa sasa VETA inafanya vizuri kwa kushirikiana ba wadau husika
wakiwemo taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuwapa mitaji
wanafunzi wanaohotimu,kutoa masomo ya ujasiriamali ,tumeingia mkataba na Sido,
na taasisi mbalimbali za kifedha,”alisena Maduki.
"Tunataka kuona kuwa wakulima wa mazao yetu hapa Tanzania
yanachakatwa na kuwa yanayoweza kutumika, tusingependa kuona mazao yetu
yanakwenda nje ya kiwa mali ghafi.
Lakini jambo linguine ambalo limenifurahisha ni kuona vijana
wanaweza kutumia kile walichojifunza darasani, hiyo ni hatua kubwa ambayo
inatia moyo kwa mzazi na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment