Saturday, July 6, 2019

Magogo ya kukatia nyama yanazalisha wadudu, atakayekutwa anatumia baada ya Septemba 30 kukiona







Ofisa Usajili wa bodi ya nyama nchini,  Sosthenes akifafanua jambo kww wananchi waliotembelea banda la bodi hii katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.


Na Selemani Magali; Dar es salaam

Imeelezwa kuwa  mwisho wa kutumia magogo ya kukatia nyama ni Septemba 30, 2019, yeyote atakayekutwa anatumia baada ya tarehe hiyo kukiona.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mtaalamu kutoka bodi ya Nyama Tanzania amesema hatua imekuja kwa sababu magogo hayo yanamadhara kiafya, ambayo yanatengeneza mazingira ya kuzaliana kwa wadudu  au vimelea vya magonjwa.

Aidha, amesema magogo hayo pia yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji anapoteza Sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa  ya kukatia nyama.

Ofisa msajili kutoka bodi hiyo Bw. Geofrey Sosthenes amesema hayo Julai 5, 2019 katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.
Mtaalamu huyo amewataka wananchi hususani wanaoshughulika na uuzaji wa nyama kutembelea banda hilo ili waweze kupatiwa elimu.

Amesema watakao kaidi agizo hilo watachukuliwa hatua na Msajili wa bodi hiyo, kwa sababu tayari amekwisha ziandikia mamlaka za Serikali za Mitaa tangu  Februari, mwaka huu kwa maana ya wakurugenzi wa idara zote kuhakikisha wanaboresha maeneo yote yanayozalisha nyama ukiwa pamoja na machinjio, makalo na mabucha.

Ofisa huyo, ameongeza kuwa, hawapendi kuyatumia magogo kwa sababu yanamdhara kutokana na kwamba hayasafishiki, ukiwa unakata nyama baada ya mwezi yanakuwa ni mabaki ya muda mrefu na yanatengeneza vimelea vya magongwa ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa walaji.

Aidha, amesema, utumiaji wa magogo pia husababisha hasara kwani mtu akitumia gogo, Kumbuka anatumia na shoka, kinachotokea nyama inagawanyika.

"Kama una bucha inauza kilo 200 kwa siku unaona ni kiasi gani unapoteza, ukipiga hesabu yako kwa mwaka unapoteza sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua mashine ya kisasa ya kukatia nyama, tunawasihi kuacha kuyatumia magogo kwa sababu si salama kwa afya za watumiaji," alisema Sosthens.

Tutahakikisha tunawashauri wamiliki wa mabucha kuhakikisha wanakuwa na mabucha ya viwango ambayo yapo kwenye sheria, viwango hivyo ni pamoja na kuacha kutumia magogo jambo ambalo tumeisha lisisitiza".

Ofisa huyo pia ametoa ombi kwa wadau wote wanaojishughulisha na mnyororo wa thamani wa nyama au anayefanya biashara hiyo au msafirishaji au mfugaji ahakikishe amesajiliwa na kumiliki cheti kutoka katika bodi hiyo.

No comments:

Post a Comment