Tuesday, July 16, 2019

KILWA WATENGA MILIONI 16 KUINUA UBORA WA ELIMU.

Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kilwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG, ofisini kwake.

Mwalimu Ayub Mwakatika, Mratibu Elimu Kata ya Tingi Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Mkoani Lindi Miongoni mwa waratibu Elimu waliopatiwa Pikipiki na Mradi wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T)

............................................

 Na Hadija Omary, LINDI.


Serikali Wilayani kilwa Mkoani Lindi imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 16 kwa ajili ya kuendeleza shuguli mbali mbali zilizokuwa zikifanywa na Mradi wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ambao umekwisha muda wake ili usimamizi huo wa Ubora wa Elimu uweze kuwa Endelevu.


Hayo yameelezwa na Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya hiyo kwa niaba ya Ofisa Elimu Msingi jana Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza Blog.


Mradi huo wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ulianza mwaka 2015 Ukiwa na malengo ya Kuinua umahiri wa KKK (kusoma kuandika na kuhesabu), kuboresha mbinu za uongozi Halmashauri, maafisa elimu kata na walimu wakuu wa Shule za Msingi pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji wa taarifa mbali mbali katika Shule ambao unaisha muda wake July mwaka 2017.


Ndandavale alisema kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutoka katika Mradi huo wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Halmashauri yao imeona ipo haja ya kuendeleza shughuli hizo ili kuongeza ufauru katika shule yao.


Aliongeza kuwa fedha hizo zitatoka katika vyanzo vyao vya Ndani vya mapato katika Bajeti ya 2018/2019 ambapo zitatumika kwa ajili ya kuwezesha waratibu Elimu kata mafuta na matengenezo ya Pikipiki hizo pamoja na Semina za Walimu wa Darasa la kwanza na la pili.


Aidha, Ndandavale aliongeza kuwa tokea Mradi huo umeanzishwa mwaka 2015 umekuwa na chachu kubwa katika mabadiliko ya uongozi, ushiriki wa wazazi kufuatilia taarifa za watoto wao, kupunguza utoro kwa wanafunzi, walimu kupata mbinu mbali mbali za kufundishia hali ambayo imeongeza ufaulu kwa wanafunzi kutoka asilimia 34 mwaka 2015 hadi kufikia 64% mwaka 2018.


Kwa upande wake Mwalimu Kuluthumu Mwaibasa Mratibu Elimu kata ,Kata ya Somanga alisema kuwa Mradi huo wa EQUIP T umewasaidia Waratibu Elimu Kata kufanya ufuatiliaji na ukusanyaji wa mara kwa mara wa taarifa mbali mbali jambo ambalo huwafanya kuwa na taarifa sahihi zinazohusu Shule zao katika kata husika.


Nae Mwalimu Ayubu Mwakatika Ofisa Elimu kata, Kata ya Tingi alisema kuwa hapo awali Kabla ya kupatiwa piki piki hizo walikuwa wanalazimika kutumia baiskeli ili kufanya ufuatiliaji wa taarifa mbali mbali katika shule jambo ambalo wakati mwingine wanashindwa kuzifikia Shule zingine kutokana na umbali wa Maeneo yalipo.


Alisema mara nyingine hulazimika kutumia gharama zao binafusi ili kutembelea Shule hizo hali ambayo ilikuwa inawafanya kushindwa kuzifikia mara kwa mara shule zilizopo pembezoni kutokana na kutokuwa na fedha za kutosho

No comments:

Post a Comment