NA
HADIJA HASSAN, LINDI
Wananchi
wilayani kilwa Mkoani Lindi Wameshauriwa kuhudhuria klinik na kuelewa afya zao
kwa undani kabla ya mama kuwa mjamzito ili kuepusha matatizo yanayojitokeza
kipindi cha ujauzito ambayo yangeweza kuzuilika kabla ya kutokea.
Ushahuri
huo umetolewa na Anjelina Abraam muuguzi mkunga kitengo cha Baba Mama na Mtoto
wa kituo cha afya kilwa masoko , kilichopo wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Abraam
Alisema ili kulinda afya ya Mama Mjamzito pamoja na Mtoto anayetarajiwa
kuzaliwa ni vyema wazazi kuanza kuhudhuria katika kituo cha kutolea huduma za
afya ya uzazi miezi mitatu kabla ya kuamua kupata mtoto ili kuweza kumlinda
mtoto atakaezaliwa.
Alisema
hatua hiyo pia itamsaidia mama mjamzito kuuandaa mwili wake kupokea kiumbe
anachokitarajia kwa kupewa ushahuri na wahudumu wa Afya waliokaribu nae.
Aliongeza
kuwa jamii kubwa ya wananchi wanaoishi maeneo hayo huwa wanahudhuria kliniki
baada ya mama kubaini kuwa ni mjamzito jambo ambalo kiafya linaweza kuwa sio
salama kwa Mama mwenyewe na hata kwa Mtoto atakae zaliwa.
“jamii
kubwa ya Wanawake wa Kilwa hupenda kuhudhuria klinik baada ya kugundua kuwa ni
mjamzito na wakati mwingine huja kwa kuchelewa na hata baada ya kujifungua
ndipo wanakuja kupata huduma za uzazi wa mpango.
Pia
alisema changamoto kubwa kwa Baba na Mama wasipohudhulia katika vituo vya afya
Mara nyingi huwenda wakawa na Magonjwa ya zinaa ambayo hupelekea mimba kuharibika
ama ukawa ni mwanzo wa kuugua kwa mama huyo baada ya kubeba ujauzito hivyo ni
vyema kuwahi kinki mapema ili kukabiliana na hali hiyo pindi utakapogundulika
kuwa unatatizo hilo.
Nae
Amina Mwaya Mkazi wa kilwa Masoko alisema kuwa kwa mara ya kwanza anahudhuria
kliniki alishauriwa na Daktari baada ya kuugua siku kadhaa na kwenda Hospitali
kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa mjamzito.
Alisema
baada ya hapo alilazimika kuhudhuria Klinik kila Mwezi ili kujua maendeleo ya
mtoto aliye tumboni huku akisema kuwa mahudhurio hayo ya klinik yalimsaidia
kujua tarehe zake za kujifungua ambazo zilikadiriwa na watoa huuma wa kituo
hicho.
Shafihi
Hamisi ni miongoni mwa wanaume wachache wa Wilaya ya kilwa wanaowasindikiza
wenza wao kwa ajili ya kupata huduma ya uzazi katika kitengo cha Baba Mama na
Mtoto katika Kituo cha Afya cha Kilwa Masoko ambapo alisema kuwa suala la
wanaume kushiriki na weza wao wanapokuwa wajawazito ni la muhimu kwa kuwa
wanaweza kufahamu afya zao kwa pamoja na namna ya kumlinda na maradhi mtoto
wanaemtarajia kumpata.
Alisema
wanaume wengi hawapendi kwenda Kliniki pamoja na wenza wao kwa kuhofia
msongamano wa wanawake katika maeneo hayo pamoja na dhana potofu ya kuwa jukumu
la kwenda kliniki ni la mama peke yake jambo ambalo sio kweli.
Hata
hivyo Hamisi ametowa Wito kwa akina Baba kujenga tabia ya kwenda na Wenza wao
klinik kwa kuwa usimamizi wa afya ya familia ni jukumu la watu wote
No comments:
Post a Comment