MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AUNGURUMA PWANI ASEMA DHAMIRA KUBWA YA CCM NI KUWAHUDUMIA WANANCHI
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AUNGURUMA PWANI ASEMA DHAMIRA KUBWA YA CCM NI KUWAHUDUMIA WANANCHI
Na Victor Masangu,Pwani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema kwamba chama cha mapinduzi (CCM) ambacho ndio kipo madarakani lengo lake kubwa ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na kuendelea kushirikia bega kwa bega na viongozi wengine katika suala zima la kuwaletea chachu ya maendeleo na si vinginevyo.
Makamu wa pili wa Rais huyo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa fupi ya kwenda kujitambulisha rasmi kwa baadhi ya viongozi wa chama pamoja na serikali baada ya kuteuliwa kuwa mlezi mpya wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani na kuahidi kushirikiana bega kwa bega katika suala zima la kukijenga chama ikiwa sambamba na kuwahudumia wananchi kutoka maeneo mbali mbali.
Aidha Makamu huyo wa pili wa Rais amewahakikishia kutowaangusha hata kidogo wanachama wote pamoja na viongozi mbali mbali kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani na badala yake watashirikiana kwa hali na mali katika kukijenga na kukiimarisha chama.
Ndugu, Hemed amewahakikishia wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Pwani kuwa atayaendeleza yale yote mazuri yaliyofanywa na aliyekuwa mlezi wa Mkoa huo na kuahidi kwamba dhamira yake kubwa ni kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinazidi kukua na kuimarika ndani ya Mkoa huo.
Amefahamisha kuwa kutokana na Maendeleo makubwa yanayofanywa na Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 Watanzania wamekuwa na Imani kubwa na chama cha Mapinduzi jambo amablo linaipa nguvu CCM ya kushinda katika uchaguzi na kuendelea kushikilia dola.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo ameahidi kumpatia mashirikiano makubwa Mlezi huyo kwa kipindi chote atakachohudumu ndani ya Mkoa wa Pwani.
Nyongo amesema kuwa Mkoa wa Pwani umekuwa ukipiga hatua kubwa kimaendeleo na kuwataka wananchi Mkoani humo kuendeleza umoja na mshikamano baina yao sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayojengwa ndani ya mkoa wa Pwani.
Kwa upande wake Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Nicas Mawazo hakusita kumpongeza Makamu huyo wa pili wa Rais kwa ujio wake na kuahidi kumpa sapoti na ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kuwatumikia wananchi.

Comments
Post a Comment