NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Bei
ya Ufuta kwenye Mnada wa 5 wa Chama Cha Ushirika cha Lindi Mwambao
Kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Lindi, Kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani
humo imeendelea kuimarika kutoka Tsh. 2,735 kwa Bei ya juu na Tsh. 2,730 Bei ya
chini katika Mnada wa Nne hadi kufikia Tsh. 2,830/= kwa Bei ya juu na Tsh.
2,825/=kwa Bei ya chini.
Akielezea
mwenendo wa Bei za Ufuta katika mikoa inayolima zao hilo Mrajisi msaidizi wa
vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi Robert Nsunza alisema kuwa ukilinganisha na
Mikoa mingine inayolima zao hilo Mkoa wa Lindi umekuwa ukipata Bei nzuri kuliko
mikoa mingine.
Alisema
katika minada iliyopita Mkoa wa Mtwara uliuza ufuta wao kwa Bei ya Tsh. 2690
kwa kilo Moja, Pwani iliuza kwa Tsh. 2700 Huku Mkoa wa Kondoa ukiuza ufuta wao
kwa Bei ya Tsh. 2683.
Nsunza
aliongeza kuwa kulingana na soko la zao hilo kwa sasa huenda Bei hizo
zikaendelea kuimarika zaidi ambapo Nchini China kwa sasa ufuta unanunuliwa kwa
Dola1800 kwa tani.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Rashidi Masudi aliwataka wakulima
wa zao hilo kuongeza umakini katika kusafisha ufuta wao ili kuendelea kupata
Bei nzuri.
Alisema
Bei nzuri wanazoendelea kuzipata ni kutokana na wanunuzi kuridhishwa na ubora
wa Ufuta wao hivyo ni vyema kuendelea kuzingatia Usafi katika ufuta unaopelekwa
kwenye Maghara yao kwa ajili ya kuupeleka kwenye Mnada
No comments:
Post a Comment