Sunday, July 7, 2019

Mtafiti abuni kitasa kinachofunguliwa na simu






CHRISTINA GAULUHANGA – DA ES SALAAM
Mtafiti kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Filbert James, amebuni kitasa cha mlango wa nyumba kinachofunguliwa kwa simu ya mkononi ili kukomesha utumiaji funguo bandia.
Akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG  katika Maonyesho ya Sabasaba leo Jumamosi Julain 6, Filbert amesema kukamilika kwa mfumo huo kutasaidia pia kuepukana na suala la uvunjaji kufuli.
Amesema mfumo huo unasaidia kufungua geti la mlango unaotembea ambapo mtumiaji akishaingia geti hujifunga lenyewe.
“Ili kupata mfumo huu ni la lazima uwe na mlango wa kutembea na mota halafu unaingiza simu kadi ambayo ndio itakuwa inakuruhusu kama unafahamu namba yake ya simu na ukichukua namba nyingine kiholela inagoma hadi ile uliyoitambulisha kwenye mfumo,” amesema.

No comments:

Post a Comment