Thursday, July 18, 2019

WAFANAYAKAZI JKCI WAMPONGEZA PRF. JANABI KWA KUTEULIWA KWA MARA YA PILI KUONGOZA TAASISI HIYO.


Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Justina Lugali akimpatia ua la pongezi lililotolewa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu kuanzia Julai 16, 2019.Picha na JKCI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikata keki iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu kuanzia Julai 16, 2019.


No comments:

Post a Comment