Afisa Mfawidhi kutoka Brela kanda ya kusini
ambaye ni mtaalamu wa mfumo wa usajili Francis Mwakalebela aliyesimama akitoa
maelekezo kwa kwa njia ya vitendo washiriki wa mafunzo hayo kuhusina
na namna ya kuweza kusajili makampuni ya na majina ya biashara kwa njia
ya mtandao.
...................................
VICTOR MASANGU, PWANI
BAADHI
ya wafanyabiashara Mkoani Pwani ambao kwa kipindi cha muda mrefu
waliokuwa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kufanyiwa vitendo vya
utapeli pindi wanapotaka kupatiwa usajili wa makampuni yao
pamoja na majina ya biashara hatimaye wamepata ufumbuzi baada ya
kupatiwa mafunzo maalumu kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)
kwa lengo la kujifunza sheria na taratibu za usajili.
Wakizungumza
katika ufunguzi rasmi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa kwa umma juu ya
kujifunza jinsi ya kutumia mfumo wa usajili wa makampuni na majina ya
biashara baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Abdala Ndauka na Elina Mgonja
wamesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya utapeli hivyo
kujikuta wanaingia hasara kubwa katika zoezi zima la upatikanaji wa leseni.
Aidha
wafanyabiashara hao wametoa pongezi kwa Brela kwa kuwapatia mafunzo hayo
ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa
zikiwakabili katika siku za nyuma katika kutekeleza majukumu yao
hususan kuweza kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashara
zao.
“Kwa
kweli sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani tunatoa pongezi zetu za dhati
kwa mamlaka husika ya Brela kwa kuona umuhimu ya kutupatia mafunzo hayo ya
kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao, maana hapo awali tulikuwa tunapata usumbufu
mkubwa na wakati mwingine kutapeliwa na baadhi ya watu hivyo kwa sasa tunaweza
kutimiza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu,”walisema wafanyabiashara hao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka Wakala wa usajili wa biashara
na leseni (BRELA) Bakari Mketo alibainisha kwamba lengo la kuandaa
mafunzo hayo kwa wafanyabiashara pamoja na umma kuhusina na kupata huduma
za usajili kwa njia ya mtandao ikiwemo kuwajengea uwezo katika suala zima la
ulipaji wa madeni kwa wateja wao ili kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata.
“Lengo
letu kubwa kwa sasa tunazunguka katika mikoa mbali mbali na kwa sasa tumeamua
kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani ili tuweze kuwapa mafunzo
maalumu ambayo yatawawezesha kuweza kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao
pamoja na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusiama na utoaji wa leseni za
viwanda,”alisema Mketo.
Pia
alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza
kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa
zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kufanya usajili wa
makampuni yao pamoja na majina ya biashara zao bila ya kuwepo na usumbufu
wowote.
Naye
Afisa biashara mkuu kutoka Wizara ya viwanda na bishara Jane Lyatuu
aliwataka wafanyabishara wote nchini kuhakikisha wanazisajili biashara
zao zote pamoja na makampuni, taasisi, na viwanda kwa lengo la kuweza
kuhimili ushindani uliopo katika soka la bara la afrika kwa kuzingatia
ubora wa bidhaa zinazotengezwa nchini.
KATIKA
mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku mbili yalitolewa kwa umma juu ya
kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashra, pamoja na alama za
bishara na utoaji wa leseni za viwanda yamewashirikisha wadau mbali mbali wa
maendeleo, maafisa biashara, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, maafisa
maendeleo, mkaguzi wa ndani pamoja na wanasheria.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani
wakiwa katika zoezi la kujifunza jinsi ya kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa
mtandao.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka maeneo mbali
mbali ya Mkoa wa Pwani wakiwa wanaelekezana jinsi ya kuweza namna na
kujisajili makampuni na majina ya biashra kwa kwa kutumia njia ya
mtandao.
Wafanyabishara wa Mkoa wa Pwani wakiwa
katika mafunzo ya kujifunza namna ya kusajili makampuni na majina ya biashara
kwa njia ya mtandao.
Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya mji Kibaha Lea Lwanji kushoto akiwa na mshiriki mwenzake wakiwa wanafuatilia kwa umakini mafunzo ya usajili kwa kutumia mfumo wa njia ya mtandao.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wanaangalia
jinsi ya mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi.
(PICHA
ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment