Na
Hadija Hassan, Lindi.
Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi imetenga julma ya Tsh. 12,000,000. Kwa ajili ya
kumaliza migogoro yote ya mipaka ya Aridhi iliyonayo hivi sasa katika vijiji
vinne ifikapo 2020.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Renatus Mchau hivi
karibuni alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza blog ofisini kwake.
Alisema
fedha hizo walizotenga ni kwa ajili ya kuwawezesha wataalamu wa Aridhi wa
Halmashauri hiyo kupima upya mipaka ya Aridhi katika vijiji hivyo.
Mchau
alivitaja Vijiji vinavyokabiliwa na Migogoro hiyo ya mipaka ya Aridhi kuwa ni
Namayuni, Mingumbi , Liwiti na likawage Alisema kuanzia mwezi January mpaka
kufikia mwezi machi kiasi cha Tsh.1,500,000. zimeshatumika katika kazi hiyo ya
upimaji upya wa mipaka ya Aridhi.
Pamoja
na mambo mengine aliiambia Bagamoyo kwanza blog kuwa licha ya kudhamiria
kutatua migogoro ya mipaka ya Aridhi pia Halmashauri hiyo inatarajia kufanya
upimaji wa stendi kuu ya Mabasi katika eneo la Nangurukulu na Mihani.
Aliongeza
kuwa upimaji huo wa Stendi kumbwa ya mabasi utawezesha upatikanaji wa ramani na
hati za Stendi mwaka 2020 ambao umeghalimu Tsh. 4,500,00
No comments:
Post a Comment