Mwandishi Wetu
Kampuni ya Puma Energy Tanzania imesema
itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi
mbalimbali ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali nchini.
Pia kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani
kwa zaidi ya wanafunzi 4500 katika shule tano za msingi Jijini Dodoma huku
ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili
kuhakikisha inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa
wengine.
Akizungumza leo Julai 25 jijini Dodoma mbele
ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana,
Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah,
amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa jiji hilo ilihusisha mafunzo ya
usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi 4500, katika shule tano
“Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini
Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa jiji hili ambapo shughuli za kijamii
na ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto
wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani,” amesema.
Dhahana amebainisha lengo ni kuwafanya watoto
kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili kuongeza uelewa kuhusu dhima nzima
ya usalama barabarani kwa Watanzania.
“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili
kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima. Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza
katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia jeshi la
Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,” amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amesema Puma Energy
Tanzania ni kampuni iliyoamua kutoa elimu ya usalama barabara nchini huku
akitoa ombi kwa kampuni hiyo kufundisha walimu ili wakifundisha masomo ya
kawaida wawe pia wanataka na elimu ya usalama.
“Nimesikia ombi la walimu na wanafunzi la kuhitaji alama za barabarani, hivyo Serikali itaendelea kuweka alama hizo pia nimezungumza na wenzetu wa Puma wamekubali kupaka rangi za usalama barabarani na wataanza na shule tano ambazo zimepatiwa elimu hii ya usalama barabarani,”amesema Mavunde.
No comments:
Post a Comment