Baadhi
ya wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma katika shule ya Kibaha
sekondari mkoani Pwani wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao ya
kawaida kwa ajili ya kujiandaa na mitihani yao mbali mbali ya majaribio na ule
wa Taifa.
..................................
VICTOR MASANGU, PWANI
SHULE
kongwe ya wavulana ya vipaji maalumu ya Kibaha sekondari iliyopo
Mkoani Pwani licha ya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika
matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka wa 2018 na kushika nafasi ya sita
kwa mwaka 2019 bado wanafunzi wake kwa sasa wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya ukosefu wa walimu ya masomo ya sayansi, uhaba wa vitabu, uchakavu wa
miundombinu ya madarasa, uhaba wa vitanda pamoja na upungufu wa matundu ya
vyoo.
Hayo
yamebaishwa na baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Jonasi Baraka ambaye ni
kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo pamoja na Kalani
Mahila ambapo wamedai kuwa serikali ya awamu ya tano inapaswa kulivalia
njuga suala hilo kwa kuharakisha kufanya ukarabati wa majengo hayo ambayo
yanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Aidha
wanafunzi hao wamesema kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha
wanasoma katika mazingira rafiki ambayo yatawafanya waongeze kiwango cha
ufaulu, hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwakarabatia majengo.
"vyoo
vinavyotumika kwa sasa ni vinne tu, kwa idadi ya wanafunzi vyoo vingine
vimefungwa kutokana na ubovu, na tuna uhaba wa maabara na walimu wa masomo ya
sayansi
“Kwa
sasa kwa kweli shule yetu ya Kibaha tunakabiliwa na changamoto mbali mbali
lakini kitu kikubwa tunachohitaji kutoka kwa serikali ya awamu ya tano ni
kutuboreshea sekta ya elimu kwa kutufanyia ukarabati wa miundombinu ya
majengo mbali mbali yakiwemo ya madarasani, vyoo, pamoja na mabweni ambayo kwa
hali yake kwa sasa sio nzuri yamechakaa, na sisis nia yetu ni kushika nafasi ya
kwanza kitaifa,”walisema wanafunzi hao.
Naye
mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha
Sekondari Dk. Hamisi Likuli amekiri kuwepo kwa changamoto mbali
mbali zinazowakabili wanafunzi hao, ambapo alibainisha hatua ambazo
tayari wameshazichukua ni kuimarisha huduma ya afya, kuboresha miundombinu ya
majengo na vyoo kujenga uzio pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji kwa
kuweka matanki pamoja na kuchimba kisima.
Katika
kukabiliana na changamoto hizo Mkuu wa shule hiyo ya Kibaha Chrisdom Ambilikile
ameamua kuja na mpango wa kuwakutanisha viongozi mbali mbali wa serikali
pamoja, wabunge pamoja na wadau wengine ambao wamesomea katika shule hiyo
kwa dhumuni la kufanya harambee ambayo inatarajia kufanyika Septemba 9
mwaka huu lengo likiwa ni kusaidia kutatua changamoto ambazo zinaikabili shule
hiyo kwa kipindi cha miaka mingi.
Mkuu
huyo alibainisha kuwa licha ya shule yake kushika nafasi ya sita kwa mwaka huu
katika matokeo ya kidato cha sita kitaifa lakini kiwango cha ufaulu kwa
wanafunzi kimeongezeka kwa daraja la kwanza kuwa na wanafunzi wapatao 143
waliopata divisheni 1.
“Kwa
kweli ukizungumzia kitaalamu utaona sisi shule yetu kwa matokeo ya kidato cha
sita kwa mwaka huu wa 2019 tumeshika nafasi ya sita kitaifa lakini mwaka jana
tulishika nafasi ya kwanza lakini kiwango cha daraja la kwanza kimeongezeka
sana tumepata wanafunzi 143 kwa hivyo utaona tumefanya vizuri na kuwa na nafasi
kubwa ya kuwapeleka wanafunzi wengi vyuoni,”alisema Mkuu huyo.
Pia
mikakati yetu tuliyojiwekea ni kushirikiana bega kwa began na wazazi, pamoja na
wadau wa maendeleo katika kuiboresha shule hiyo ambayo wanatarajia kukusanya
kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa jengo
kubwa la kisasa ambalo litakuwa likitumika kwa matumizi mbali ikiwemo
maktaba,kompyuta pamoja na mambo mengine yanayohusiana na elimu.
Shule
hiyo kongwe ya Kibaha sekondari yanye wanafunzi 669 na walimu 56 ilianzishwa
mwaka 1965 ambapo viongozi mbali mbali wa serikali na wabunge wameweza
kusomea hapo akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai sambamba na Free Man Mbowe Mwenyekiti wa
Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) pamoja na Razaro Nyarandu.
Mkuu
wa shule ya Kibaha Sekondari Chrisdom Ambilikile akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na mikakati mbali
mbali aliyojiwekea katika kuhakikisha anapandisha zaidi kiwango cha
elimu, pamoja na mpango wa kufanya harambee kubwa ya kuwakutanisha viongozi wa
serikali na wabunge waliosomea katika shule hiyo ili kuzitatua changamoto
zilizopo katika sekta ya ellimu.
Mkuu wa shule ya Kibaha
Sekondari Chrisdom Ambilikile akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari
hawapo pichani chumba cha maabara ambacho kimefanyiwa ukarabati na serikali kwa
lengo la kuweza kuwapa fursa wanafunzi kujifunza zaidi kwa vitendo.
Kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa
shule ya Kibaha Sekondari Jonasi Baraka akizungumzia
changamoto mbali mbali zinazowakabili katika shule hiyo pamoja na mipango
waliyojiwekea katika kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo yajayo ya
kidato cha sita.
Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha
Sekondari Dk. Hamisi Likuli akifafanua jambo kuhusiana na hatua mbali
mbali ambazo tayari wameshazichukua katika kuhakikisha wanashirikiana na
serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu katika shule
hiyo.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
No comments:
Post a Comment