Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid
Zahoro (kulia) akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya, Frank Daniel Masiaga ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kwa tiketi ya CHADEMA.
.............................
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Nyakahamba kata ya Kerege wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kwa
tiketi ya CHADEMA, Frank Daniel Masiaga amejiuzulu nafasi yake na kutangaza
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 13 julai 2019.
Akitangaza
uamuzi huo mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya
CCM kata ya Kerege, Masiaga alisema ameamua kurudisha kadi ya CHADEMA na
kuchukua kadi ya CCM kutokana na kile alichokiita ni kumuunga mkono Rais John
Magufuli katika juhudi zake za kuleta maendeleo.
Alisema
katika kipindi chote cha miaka mitano amekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kupitia
Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini amefanya kazi katika
mazingira magumu hivyo ameona ni bora ajiunge na CCM ili aweze kufanya mambo
mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
ili kuweza kuleta maendeleo katika eneo lake ameona ni vyema ajiunge na CCM
kwakuwa CHADEMA haiwezi kuleta maendeleo.
Masiaga
alisema uamuzi wake wa kujiunga na CCM umepokelewa kwa furaha na wananchi wa
kitongoji chake hali iliyopelekea wanachama 300 wa CHADEMA kurudisha kadi za
CHADEMA nakujiunga na CCM.
Akizungumza
mara baada ya kumpokea, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid
Zahoro amesema anampongeza Masiaga kwa kitendo chake cha kurudi nyumbani na
kuwataka viongozi wa CCM kata ya Kerege kumpa ushirikiano ili kuimarisha CCM katika kitongoji cha Nyakahamba.
Alisema
CCM ni kuchapa kazi hivyo wanachama wapya hao wanapaswa kuwajibika na kuahidi
kuwanunulia kadi zote mia tatu kwa fedha zake ikiwa kama motisha kwa wanachama
hao wapya waliotoka CHADEMA.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid
Zahoro, akionesha kadi za CHADEMA ambazo wanachama wake wamejiunga na CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro, (kushoto) akimpongeza mwanachama mpya,
Frank Daniel Masiaga ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kwa tiketi ya CHADEMA.
No comments:
Post a Comment