Selemani Magali
Kampuni ya chai bora imeelezea kufurahishwa kwake
na kushiriki maonyesho ya sabasaba, wakisema maonyesho hayo yamewasaidia
kuwakutanisha na wakulima moja kwa moja kuwaeleza namna wanavyoweza kufanya
kazi kwa pamoja.
Wakulima wadogowadogo walikuwa wanaogopa kampuni ya chai
bora wakizani ni kwa ajili ya wakulima wakubwa, lakini kupitia maonyesho ya
sabasaba wameweza kuondoa dhana hiyo potofu kwa wakulima.
Katika upande mwingine wakulima wa zao la Chai wametakiwa
kuendelea kulima Chai kwa wingi katika kuhakikisha Soko lake linakuwa ndani na
nje ya nchi.
Pia wametakiwa kulima aina mbali mbali ya Chai na
kuacha mazoea ya kulima aina moja ya Chai nyeusi badala yake walime aina mbali
mbali ikiwemo Chai ya maua.
Akizungumza Jana Jijini Dar as Salaam maonyesho
ya 43 ya biashara ya kimataifa ,Awatif Bushiri alisema kwa sasa wakulima
wamekuwa wakilima aina moja ya Chai hali inayowafanya watu watengenezaji wa
majani ya Chai kukosa kuweka aina nyingine ya Chai na kutumia aina moja ya Chai
nyeusi.
"Wakati mwingine tunapata shida ya
kutengeneza Chai aina nyingine Kutokana na wakulima wengi kulima Chai aina moja
na wakati mwingine uwa tunaamua kuagiza nje ya nchi Chai za maua ambazo
zinakuwa na harufu za matunda mbali mbali," alisema
Bushiri alisema zao la Chai linasoko kubwa ndani
na nje ya nchi hivyo wakulima wakiongeza jitihada tutaweza kuzidisha kupiga
hatua katika kufanya biashara na kujitangaza zaidi kwa nchi za nje.
"Sisi Chai Bora tumekuwa tukiuza bidhaa zetu
hadi nje ya nchi na sasa tumefikia katika nchi tano ambazo tumekuwa tunauza
Chai yetu,ikiwemo Ghana,Saudi Arabia,South Africa,Rwanda na Kenya ,"
alisema Bushiri
Kwa Mwaka huu Banda la Chai Bora limeshika nafasi
ya kwanza katika kipengele cha Chakula,Dawa na Vinywaji katika maonyesho hayo.
No comments:
Post a Comment