Na Selemani Magali; Dar es Salaam.
Wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela) imesema itashiriki
kwa nguvu zote katika maonyesho ya nanenane ya mwaka 2019, msisitizo ukiwa ni
kuwahamasisha wananchi kurasimisha shughuli zao za uzalishaji ikiwamo mifugo,
kilimo na uvuvvi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu afisa Mtendaji Mkuu wa Brela
Emmanuel Kakwezi amesema Brela imejipanga vizuri kutoa elimu kuhusu shughuli
zinazofanywa na wakala, na kwamba watawashashiwi washiriki na raia
watakaotembelea maonyesho hayo juu ya umuhimu wa kurasimisha shughuli zao
Mbali ni dhima ya kuwashauri wananchi kuhusu kurasimisha
shughuli zao ambazo mara nyingi zimkuwa zikitumika kwa matumizi ya nyumbani,
wanaamini baada ya elimu hiyo watabadilika na kusajili shughuli zao ili
ziwaletee manufaa Zaidi.
“Kipindi hiki brela itakuwa inatoa huduma zake palepale viwanja
vya simiyu, Brela itakuwa inatoa huduma zake zote ikiwamo kusajili makampuni,
kusajili majina ya biashara, kutoa leseni, kusajili alama za biashara kutoa hati
na leseni za viwanda,” alisema Kakwezi
Amesema wanataka kuona shughuli uvuvi, kilimo na ufugaji
haziishi kukidhi haja ya matumizi ya nyumbani tu, zinatakiwa ziwe shughuli za
kibiashara, Brela itawawaeleza utaratibu namna wanavyoweza kusajili makampuni
na kuwasaidia namna ya kupata masoko.
Amesema Brela imejipanga
vizuri, tayari wana business portal (mfumo wa kuuza bidhaa nje ya nchi),
watatoa elimu hiyo ili kuwafanya jamii ijue namna gani wanavyoweza kuuza bidhaa
zao nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkurugenzi ametoa wito kwa Wananchi kutembelea banda la Brela
kwa sababu limesheheni wataalamu ambao watawasaidia kupata maelezo yote
yanayohusu huduma zinazotolewa na Brela
pamoja na kupata elimu ya kurasimisha shughuli zao.
“Wananchi wote watakaofanikiwa kufika katika maonyesho ya
mwka huu wahakikishe wanapita katika
banda la Brela ili kujipatia elimu.
Tutawaeleza utaratibu wa kuweza kusajili makampuni, tuwaonyeshe
namna gani wanaweza kupata leseni, lakini pia kuwaeleza namna watakavyoweza
kupata soko zuri kwa kuuza bidhaa zao,” alisema
MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA NANENANE 2019
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Mjini
Bariadi kuanzia tarehe 29/07/2019 hadi 08/08/2019.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema maonyesho hayo yatakuwa ya tofauti sana ukilinganisha nay
a mwaka jana, kwa sababu wamefanikiwa kuboresha baadhi ya mambo ikiwamo utoaji
wa semina, warsha kwa washiriki wote wa maonyesho hayo.
Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais atafungua rasmi maonesho hayo
Agosti Mosi, 2019 na kwamba jumla ya waonyeshaji 300 tayari wameshajiandikisha
kushiriki maonyesho hayo.
“Taasisi, Mashirika mbalimbali na wajasiriamali wataanza
kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao Julai 29, 2019, nataka nitumie nafasi
hii kawashauri wajasiliamali, wafanyabiashara, wakulima, wavuvi, wafugaji
kujitokeza kwa wingi katika maonyeshoya mwaka huu, tumeyaboresha sana na kuna
vitu vingi vyenye tija” Alisema Mtaka
Amesema maonyesho hayo yatakaribisha viongozi wa Kitaifa, Agosti
03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri Mkuu, Agosti 06, 2019 tutakuwa na Waziri Mkuu
Mstaafu, Mizengo Pinda na kilele chake yanatarajiwa kutembelewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye
atayafunga maonyesho hayo..
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema ameridhishwa
na maandalizi ya Maonesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Simiyu na kutoa wito
kwa wakulima na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
maonesho haya ili kuja kujionea teknolojia mbalimbali zitakazojibu changamoto
za wakulima, wafugaji na wavuvi.
Aidha, Mhe. Mgumba ametoa wito kwa waoneshaji kuwa wabunifu
katika teknolojia, huduma na bidhaa watakazoonesha ili maonesho haya yawe
chachu ya kuwasaidia wakulima, wavuvi na wafugaji kuongeza tija katika
uzalishaji
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuwa na
maonesho ya tofauti na mwaka jana, lengo likiwa ni kuifanya kanda hiyo kuwa ni
mahali pa kudumu pa wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa na maonesho ya kilimo
biashara.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili sasa
mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili yaani, Kanda
ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa Magharibi(Mwanza,
Geita na Kagera) ambapo mwaka huu yanaadhimishwa chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO,
MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”
No comments:
Post a Comment