Thursday, July 11, 2019

HALMASHAURI YA KILWA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 4 KUREJESHA MAZALIA YA SAMAKI BAHARINI.

Na Hadija Hassan, Lindi.


Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi imetumia kiasi cha Tsh.4,350,000 kwa kwa ajili ya kurejesha mazalia na makalia ya Samaki yaliyoharibika kutokana na shughuli mbali mbali za kibinaadamu.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo jana alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza blog ofisini kwake.


Alisema kuwa fedha hizo zimetumika kwa kipindi cha miezi mitatu January hadi march mwaka 2019 Huku akieleza kuwa katika kiasi hicho cha fedha sh.350,000 zilitumika kwa ajili ya uimarishaji na uanzishwaji wa vikundi vya ushirika wa Uvuvi na wafugaji wa samaki 650,000. kurejesha mazalia na makalia ya samaki yaliyohalibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na uharibifu wa mazingira kwa kuweka Matumbawe bandia pamoja na kupanda Mikoko katika Bahari.


Mchau alisema Mpaka sasa tayari Miamba Mitano ya Chocha ndogo, chocha kubwa, pera, nyuni na mpovi imefungwa kwa ajili ya kurejesha mazalia ya samaki kwenye kata za Somanga, Kivinje, Songo songo na Singino.


Aidha, Mchau aliongeza kuwa, Tsh. 950,0000,00 zilitumika kwa ajili ya kuendeleza Mapambano dhidi ya Uvuvi haramu pamoja na kuufanya Uvuvi halali kuwa endelevu na wenye tija ambapo doria tatu(3) za kupambana na uvuvi haramu zilifanyika.


Alisema katika Dolia hizo tatu zilizofanyika mbili zilifanikiwa kukamata nyavu haramu za tamba 4, saratonga2, kokoro 18 nyavu chini ya 8mm.

No comments:

Post a Comment