NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Lindi imeanza uchunguzi ili
kubaini matumizi ya fedha Tsh. 221,000,000, zilizotolewa na Serikali kwa ajili
ya Ukarabati wa Baadhi ya Majengo katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa huo Sokoine.
Hayo
yameelezwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Lindi Stephen chami jana alipokuwa
anatoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zao katika kipindi cha miezi mitatu
kuanzia mwezi Aprili hadi juni mwaka 2019.
Chami
alisema kupitia dawati lao la utafiti na udhibiti limebaini mapungufu makubwa
kwenye ukarabati wa Hospitali hiyo ambapo marekebisho hayo yalihusisha ujenzi
wa Wodi ya Watoto, Choo cha wagonjwa pamoja na matenk mawili ya maji ya Lita
50,000 na lita 150,000.
Alisema
kupitia Dawati hilo TAKUKURU ilibaini kuwa fedha za ukarabati huo zimekwisha
wakati ukarabati huo haujakamilika na baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili
ya ukarabati huo pamoja na kutokuwepo na maelezo yoyote juu ya upotevu huo.
Chami
aliongeza kuwa kufuatia hali hiyo TAKUKURU Mkoa wa Lindi kupitia Dawati lake la
Uchunguzi na mashtaka limeshaanza uchunguzi wa kina ili kubaini waliohujumu
ukarabati huo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Nae
Ofisa Uchunguzi na Ukaguzi wa Miradi , TAKUKURU Mkoa wa Lindi Michael Manento
alidai kuwa Kwenye bajeti ya 2017/2018 hospitali hiyo iliomba fedha sh. 300,000,000.
Kwa ajili ya ukarabati wa jingo la utawala, chumba cha X-ray, pamoja na wodi
ambapo hata hivyo walipatiwa kiasi cha Tsh. 221,000,000,.
“kwa
sababu pesa ilikuja pungufu wao kama menejiment ya Hospitali waliamua kufanya
kazi tatu kujenga wodi ya watoto, Vyoo vya Wagonjwa wa nje pamoja na Matank
mawili ya maji, hivyo wakati tunakagua kazi ile kulingana na BOQ zao pamoja na
manunuzi ya vifaa walivyoandika tukabaini kwamba bajeti iliyowekwa na fedha
iliyokuja fedha imeisha kabla ya kazi kukamilika” alifafanua.
Hata
hivyo Manento Alizitaja kazi ambazo hazijakamilika katika ukarabaiti huo ni
pamoja na ujenzi wa Wodi ambao umefikia hatua ya kupauwa pamoja na vifaa ambayo
vinaonekana vimenunuliwa lakini havionekani vilipo
No comments:
Post a Comment