WANANCHI ELFU 30 MANISPAA YA KIBAHA WAPATA NEEMA KUBWA  YA MSAADA WA KISHERIA 

Na Victor Masangu,Kibaha 

ZAIDI ya wananchi wapatao  elfu 30 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani  wamefanikiwa kupatiwa  huduma za msaada wa kisheria bure kupitia  Kampeni  ya  Mama  Samia  awamu ya pili na kupata fursa ya kusaidiwa mambo mbali mbali yakiwemo utatuzi  wa migogoro mbali mbali ikiwemo ardhi,ndoa, ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake   pamoja na kupatiwa ushauri na elimu ya masuala ya kisheria  

Hayo yamebainishwa na Wakiri wa serikali kutoka Wizara ya katiba na sheria Kasilida Chimagi wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na mwenendo mzima kuhusiana  na  zoezi la kampeni hiyo  ambapo amebainisha kwamba wananchi wengi wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuweza kupatiwa huduma hiyo.

Amesema kwamba katika zoezi hilo la kuwasikiliza wananchi wameweza kubaini kuwepo kwa changamoto mbali mbali za  migogoro ya ardhi ambapo pia wameweza kutoa ushauri na elimu.

"Tangu tuanze kampeni yetu hii ya msaada wa kisheria tunaendelea vizuri na tumefanikisha kuwapatia msaada wa kisheria zaidi ya wananchi elfu 30 katika Halmashauri ya Manispaa ya  Kibaha,"amebainisha


Nao baadhi ya wanawake katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  ambao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kuweza kupata msaada huo  wa kisheria  akiwemo Judith Mwasha wamemshukuru kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni hiyo ambayo imeweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kutatua  changamoto zao.


Naye mmoja  wa mwanamama  ambaye anakabiliwa na changamoto ya kutelekezwa  na mume wake akiwa na watoto watatu  Eva Ombela  amesema kwamba ujio wa kampeni hiyo ya msaada wa sheria awamu ya pili ana imani itaweza  kumsaidia kwa kiasi kukubwa  kupata haki zake zote za msingi.

 
Kampeni ya msaada wa kisheria awamu ya pili  ya Mama Samia katika Mkoa wa Pwani  ilizinduliwa rasmi tangu Octoba 28 mwaka huu na Waziri wa katiba na sheria Abdalah Ulega kwa lengo la  kuweza kusikiliza  na changamoto  mbali mbali zinazowakabilii wananchi.

                                                        MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016 HAYA HAPA

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

KATIBU MKUU MALI ASILI AKEMEA UINGIZWAJI WA MIFUGO KWENYE MAENEO YA HIFADHI