Na
Hadija Hassan, Lindi.
WAZIRI
Mkuu Kassimu Majaliwa amepokea msaada wa vifaa Tiba kutoka Shirika lisilo la
Kiserikali la Helping Hand for Relief and Development (HHRD) inayojihusisha na
utoaji huduma na Misaada kwa Maendeleo ya wananchi.
Vifaa
vilivyotolewa ni vitanda vya kujifungulia akina mama wajawazito, Magodoro, Mashine
za Matibabu na vingine mbali mbali kwa ajili ya kutolea huduma kwa wananchi
wanao kwenda vituo vya kutolea tiba katika Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi.
Akikabidhi
vifaa hivyo ambavyo thamani yake inafikia Dola za Kimarekani 100,007 sawa na
fedha za Kitanzania Sh,milioni 250. kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mbunge
wa Ruangwa, Mwenyekiti wa wa Bodi ya taasisi hiyo, Yassir Salim Awadhi alisema
ni moja ya kazi ya taasisi yao kuunga mkono juhudi za Serikali.
“HHRD
ni wadau wa Maendeleo na ni mashuhuda kwa Serikali ilivyo na mikakati ya
kuibadilisha Taifa hili liweze kusonga mbele katika Sekta zote, viwanda, Afya
na Elimu ”Alisema Awdhi.
Mwenyekiti
huyo alisema msaada huo utakuwa unasaidia katika kuboresha Afya kwa wananchi wa
Wilaya ya Ruangwa na Tanzania kwa ujumla bila ya kujali itikadi walizonazo,huku
akisisitiza kuendelea kushirikiana na Serikali katika masuala ya Maendeleo.
Awadhi alisema Shirika hilo,lisilo la kiserikali lenye makao makuu yake nchini
Marekani, na Afrika hufanya kazi katika nchi (16), Ofisi ndogo ipo Nairobi
nchini Kenya na kwamba hujishughulisha zaidi na changamoto za kijamii, wakiwemo
yatima katika Sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na matukio ya dharura.
Pia,
alisema kwa Tanzania Shirika hilo la (HHRD) limejikita katika miradi
mbalimbali, ikiwemo msimu wa ugawaji Nyama na Chakula kwa Jamii kipindi cha
Mafuriko na kile kpindi cha maujaji wanaoenda Hijja.
Aidha
alisema Shirika hilo kwa sasa linahudumia watoto yatima (250) Wilaya ya
Kisarawe, Mkoani Pwani kwa kulipiwa mahitaji ya Shule, vikiwemo vifaa, Sare, Vitabu,
Makazi, Chakula na Nguo za Sikukuu, upimaji Afya, Mafunzo na Malezi kwa wazazi
na walimu.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na Mbunge wa Ruangwa amelishukuru Shirika la (HHRD) kwa
msaada uliotolewa, huku akiendelea kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhudumia watanznia.
Majaliwa
alisema msaada huo utakaogaiwa kwa vituo vyote vya Afya na Zahanati, utapunguza
usumbufu kwa wananchi wenye matatizo kufuata huduma za matibabu mbali na maeneo
wanayoishi.
Waziri
Mkuu Majaliwa yupo Wilayani Ruangwa kwa mapumziko ya muda mfupi.
No comments:
Post a Comment