Sunday, July 14, 2019

MAHDI WA PARADISE BAGAMOYO AUWAWA NCHINI SOMALIA.

Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake.
 
Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake.
.....................................

Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte, wa Tanzania ambae alikuwa mmiliki wa hoteli ya Paradise Bagamoyo ameuawa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia.


Shambulio hilo la kujitoa muhanaga limetokea ijumaa ya tarehe 12 julai 2019 katika hoteli ya Asasey iliyopo  mji  wa bandari  wa  Kismayo nchini Somalia.


Watu 26 wameripotiwa kufariki dunia katika shambulio hilo wakiwemo watanzania watatu, na wengine 56 kujeruhiwa.


Miongoni mwa watanzania watatu waliofariki ni pamoja na mmiliki wa Hoteli ya Paradise ya Bagamoyo, Mahad Nur Gurguurte na wengine wawili (2).


Aidha mbali ya kupoteza Watanzania watatu, wengine waliopoteza maisha ni raia wa Kenya watatu, Wamarekani watatu, Muingereza mmoja na Mcanada mmoja.


Watu walioshuhudia  wamesema  miongoni  mwa  waliouwawa  ni mwanaharakati  maarufu  katika  mitandao  ya  kijamii  na  mwandishi habari  wa Somalia.


Ndugu wa  mwandishi  habari Mohamed Sahal wamethibitisha  kifo chake  na kusema  kuwa  mwanaharakati  katika  mitandao  ya kijamii  Hodan Naleyeh  na  mume  wake  pia  wamefariki  katika mripuko  huo.


Chama cha  waandishi wa habari nchini  Somalia  SJS kimethibitisha kifo  cha  mwandishi  huyo.


"Ni  siku  ya masikitiko makubwa  kwa  waandishi  habari  wa  Somalia," katibu  mkuu  wa chama  hicho  Ahmed Mumin  alisema  katika  taarifa yake.


Kwa mujibu  wa  vyanzo kadhaa, wengi  wa  wale  wanaoishi katika hoteli  hiyo walikuwa  ni  wanasiasa  na  wafanyabiashara  kabla  ya uchaguzi  ujao  wa  kimkoa.

Jengo la hoteli hiyo kama linavyoonekana mara baada ya kushambuliwa.

No comments:

Post a Comment