Sunday, July 7, 2019

JAHAZI ZAKAMATWA BAGAMOYO KWA KUBEBAA MKAA WA MAGENDO.






Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfan, akimuonesha Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Bi kasilda Mgeni, Majahazi yaliyokamatwa kwa kubeba mkaa wa magendo, majahazi hayo yalikamatwa Bandari bubu ya mto shanga kitongoji cha RAZABA kata ya Makulunge wilayani humo.

....................................


Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) wilaya ya Bagamoyo, wamekamata majahazi mawili yaliyobeba mkaa gunia zaidi ya mia mbili katika Bandari bubu ya mto shanga, kitongoji cha RAZABA kata ya makulunge.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, amewataka wananchi wilayani humo kufuata sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu ili kuepuka usumbufu ambao wanaweza kuupata.

Akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio katibu tawala huyo alisema watakaokiuka sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu serikali itawachukulia hatua za kisheria.

Alisema kutofuata sheria katika uvunaji wa misitu kunapelekea uvunaji holela jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa mazingira.

Alisema misitu inahifadhiwa kwaajili ya utunzaji wa mazingira hivyo shughli zote za uvunaji wa mazao ya misitu ni lazima zifuate sheria na kupata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa misitu.

Aliongeza kwa kusema kuwa, uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uvunaji holela utapelekea kuwa na maeneo yenye majangwa na kukosa mvua kwa wakati jambo ambalo pia litasababisha ukame wa mazao ya binadamu na wanyama.

Aidha, alibainisha kuwa, utoroshaji wa mazao ya misitu unapelekea pia kuikosesha serikali mapato ambayo kimsingi ndiyo yanategemewa kuleta maendeleo katika jamii.

Alisema serikali haikatazi wananchi kufanya shughuli zao lakini kinachotakiwa ni kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili mwananchi ajiongezee kipato, mazingira yatunzwe huku serikali ikiwa inainaingiza mapato kwaajili utekelezaji wa huduma za jamii.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfani amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 na muongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2017.

Alisema kukamatwa kwa majahazi hayo ni muendelezo wa doria zinazofanywa na kikosi cha TFS kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ili kubaini watoroshaji wa mazao ya misitu.

Hivi karibuni Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Bagamoyo walifanya semina elekezi kwa watumiaji wa majahazi na bodaboda zinazobeba mkaa ili kuwafahamisha sheria za usafirishaji wa mazao ya misitu na kuwasisitiza kufuata sheria.

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akizungumza na waaandishi wa habari eneo la tukio.

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akitoa maelekezo kwa Meneja wa TFS wilaya, Ally Khalfani (kushoto) mara baada ya kufika kwenye bandari bubu ya mto shanga iliyopo kitongoji cha RAZABA kata ya makulunge, eneo hilo hutumika kwa uturoshaji wa mazao ya misitu na bidhaa nyingine za magendo.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, picha ya juu kulia na picha ya chini kushoto, akiwa anavuka mito na mikondo ya bahari ya hindi ili kuelekea kwenye bandari bubu ya mto shanga kujionea utoroshaji wa mazao ya misitu katika eneo hilo.

 

Utoroshaji wa mazao ya misitu licha ya kuharibu mazingiraa pia unaoikosesha serikaali mapato.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wakielekea kwenye Bandari bubu ya mto shanga iliyopo kitongoji cha RAZABA kata ya Makulunge, kushoto ni 

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akiangalia tanuri la mkaa ambalo wahusika wa tanuri hilo hawakufuata sheria za uvunaji wa misitu na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfani


Watendaji wa TFS WILAYA YA Bagamoyo wakiwa katika eneo la tukioa baada ya kukamata majahazi mawili yaliyobeba mkaa kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment