MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),
imebuni mfumo maalumu kwa ajili ya kumsaidia trafiki kuongoza magari bila
ya kusimama katikati ya barabara.
Hapa kama mnavyoona tunalo mfano wa daraja la juu na la
chini, hizi taa mnazoziona sio za kawaida kama zile ambazo mmezizoea, hizi za
kwetu askari anaweza kuziendesha anavyotaka, dhamira ni kumsaidia askari
asigongwe lakini pia kuondoa msongamano wa magari.
Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara
Mwalimu wa magari Makubwa kutoka Veta kihonda Morogoro Mwalimu Willium Emanuel
Munuo amesema lengo la mfumo huo ni kumsaidia trafiki kuepuka kero mbalimbali
asimamapo barabarani ikiwemo kugongwa na magari.
Mwalimu Munuo amesema tayari mfumo huo umeshapelekwa
costech tayari kwa kusajilia ubunifu huu, tayari kwa mfumo huu kutumika.
Amesema wazo la kutengeneza mfumo huo liliwajia kutokana
na kuona kero iliyokuwepo katika barabara na kuona matrafiki wamekuwa wakipata
shida na kuatarisha maisha yao pindi wanapokuwa barabarani.
Amesema
mfumo utamsaidia trafiki kufanya kazi bila ya kutumia nguvu wala kusimama
katikati ya barabara hivyo kumpa urahisi zaidi wa kuangalia ni sehemu gani
ambapo pamezidiwa na foleni na kuponyeza mfumo huo kisha taa zitawaka.
"Teknolojia
hii bado haijaanza kufanya kazi tumepeleka wazo katika Ofisi husika ili waweze
kuungalia kama unaweza kusaidia kupunguza adha ya foleni," amesema Swanga.
Ameongeza
kuwa mfumo huo utafungwa pembeni ya barabara na kuunganishwa katika taa za
barabarani ambapo trafiki atakuwa akibadilisha ni sehemu gani ambapo
magari yameonekana kukaa kwa muda mrefu.
Aidha Mwalimu huyo amesema taa hizo zinatumia umeme wa
kawaida na wajua. Taa hizo zinadaiwa kuwa suluhu ya kumsaidia askari wa
barabarani.
No comments:
Post a Comment