Sunday, July 7, 2019

WANANCHI WAVUTIWA NA PIKIPIKI INAYOGUNDUA KILEVI, HAIWAKI KAMA UMELEWA, HUJAA KOFIA NGUMU AU MWENDO KASI


Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo. 

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa kofiangumu (helmet). 

Akizungumza na katika viwanja vya maonesho ya sabasaba,  mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika. 

Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki. 

Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini

No comments:

Post a Comment