Damian Masyenene, Mwanza
Mahakama Kuu
ya Tanzania Kanda ya Mwanza, imewaachia huru na kuwafutia mashtaka askari
wanane waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Askari hao walikuwa na mashtaka
12 yakiwamo ya uhujumu uchumi, kuomba na
kupokea rushwa ya Sh milioni 700, kuisababishia hasara Serikali na utakatishaji
fedha ambapo walioachiwa ni pamoja na Koplo Dani Kasara, Matete Misana,
Konstebo Japhet Kuliko, Maingu Sorry, Alex Mkali, Timoth Paul, David Ngelela na
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Moris Okinda aliyekuwa kiongozi wa askari
hao na mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo.
Uamuzi huo umetolewa
leo Alhamisi Julai 18, na Hakimu Mkazi wa
Mkoa wa Mwanza, Rhoda Ngimilanga aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, ambapo amesema
kutokana na ombi lililowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kupitia
kwa Wakili wa upande wa mashtaka, Castus Ndamgoba la kutokuwa na nia ya
kuendelea na shauri hilo.
Washtakiwa hao ni miongoni mwa wafungwa wengine
zaidi ya 200 kutoka magereza mbalimbali waliofutiwa mashtaka na kufutiwa
vifungo vyao jana baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya ghafla katika
Gereza la Butimba, mkoani Mwanza juzi.
No comments:
Post a Comment