Saturday, July 6, 2019

Hakikisheni mnaandaa bidhaa kwa ubora wa hali ya juu, acheni udanganyifu




MKURUNGEZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin  Rutageluka amewaonya  wafanyabiashara wa viungo waache udanganyifu wanapotayarisha bidhaa ili viwe katika ubora unaofaa kuweza kupata soko mpaka nje ya nchi.

Akizungumza leo katika Maonesho ya 43 ya kimataifa na biashara Rutageluka amesma, baadhi ya  wafanyabiashara hasa wa kiungo cha pilipili manga wamekuwa na tabia ya  kuchanganya mbegu za mapapai ili kuzidisha ujazo katika kiungo hicho


Rutageluka amesema, no bora wafanyabiashars wakaacha udanganyifu katika bidhaa zao lengo likiwa ni kuhakikisha viungo vya Tanzania vinatumika ndani ya Nchi na nje ya Nchi.

Amesema TANTRADE imebaini udanganyifu unaofanywa kwa baadhi ya mikoa na wafanyabiashara wamekuwa wakichanganya viungo na vitu vingine ili kuleta uzito udanganyifu ambao huwezi kuubaini mara moja.

Kwa upande wake, waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amina Salum Ali amewataka Watanzania kuthamini bidhaa zinazotengezwa ndani ya Nchi na wale wanaofanya biashara ya viungo kutengeneza viungo vyao kwa umakini ili waweze kupata soko nje ya nchi.

Amesema,  japokuwa sekta hiyo imekuwa na changamoto nyingi lakini serikali itahakikisha inazipunguza.

Akiongelea kilimo cha Mwani,  Waziri Amina aliongelea kilimo Cha mwani na kusema kuwa hivi Sasa kimekuwa na tija kwa maendeleo ya wananchi.

No comments:

Post a Comment