Na KENNETH NGELESI-MBOZI
FAMILIA ya Askofu Mulilege Mkombo Ambindwile Kameka wa Kanisa la
‘House of Preyer Shield of Faith Christian Church’ imemuomba Rais Dk.John Magufuli kuingilia kati
na tatizo na kiongozi huyo ambaye kwa sasa inadaiwa yupo mahabusu tangu Januari
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, baba mzazi wa askofu huyo, Ambilikile Kameka,
alisema anaiomba Serikali ya Rais Magufuli imnusuru kiongozi huyo wa kiroho.
Mchungaji Mwaipungu alisema askofu wao alikamatwa Jenuari 17, mwaka huu Jijini Dar es Salaam, kwa hutuma za
mashaka na urai wake na kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Machi 17, mwaka huu.
“Awali alikamatwa kwa madai kuwa si raia lakini Mahakama Kuu
ikadhibitisha kuwa ni raia halali lakini tangu wakati huo bado anashilikwa sasa
sisi hatuelewi hadi sasa. Tunamuomba Rais wetu Dk.John Magufuli na serikali
yake watusaidie suala hili,” alisema Mwaipungu
Kutokana na madai hayo mwandishi alimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mmabosasa, ambapo alimtaka mwandishi wa habari
hawe na subira wa suala hili kwani yupo nje ya ofisi.
No comments:
Post a Comment