Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde
wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna
ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya
kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda
tarehe 19 Desemba 2018.
.....................................
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha
Biashara
Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna
ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia
tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.
Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe.
Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini
taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia
ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha
biashara baina ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na
Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.
Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt
Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero
walishiriki mkutano huo.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya
No comments:
Post a Comment