Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kati kati
akiwa ameshika moja ya kompyuta ambazo zmezitoa kwa niaba ya serikali, kushoto
kwake ni Naibu waziri wa uchukuzi na Mawasialiano Injinia Atashasta Nditiye, na
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Waziri wa Tamisemi
Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika
halfa hiyo ya kukabidhi kompyuta 25 kwa shule 14 zilizopo katika halmashauri ya
Kisarawe. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
.................................................
VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZIRI wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo
amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini pamoja na maafisa
elimu kuachana kabisa na vitendo vya kuwanyima fursa walimu ambao wanahitaji
kujifunza somo la tehema na badala yake wahakikishe wanatoa vibali bila ya kuwa
na ukilitimba wowote kwa lengo la kukuza teknolojia na mawasiliano.
Jafo ametoa kauli hiyo
wakati wa halfa ya kukabidhi kompyuta 25 ambazo zimetolewa na serikali kupitia
mfuko wa mawasilino kwa wote ambapo zitazinufaisha shule za sekondari 14
zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.
Jafo alibainisha
kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawajengea
uwezo walimu ambapo hadi sasa tayari walimu wapatao 570 wameshapatiwa
mafunzo maalumu kwa ajili ya somo la tehema ili kuendana na kasi na mabadiliko
ya kiteknolojia.
“Kitu kikubwa sisi kama
serikali kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kwamba somo hili la Tehama kwa walimu
linapewa kipaumbele zaidi, lakini sipendi kuona walimu wananyimwa vibali kwa
ajili ya kwenda kuongeza ujuzi katika somo hilo hivyo kuanzia sasa ofisi yangu
italisimamia hili na kwamba wakurugenzi wote na maafisa elimu msiwanyime vibali
kabisa wapeni acheni roho mbaya,”alisema Jafo.
Naye Naibu waziri wa
uchukuzi na mawasiliano Injinia Atashasta Nditiye amesema kwamba kwa sasa
serikali imeshaanza mchakato kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo 20 vya Tehama
kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa upande wa Tanzania visiwani tayari wameshajenga
vituo vya Tehama vipatavyo 10 ambavyo ni mahususi kwa wanafunzi,
wanafanyakazi, pamoja na walimu.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwamba katika kuunga mkono juhudi za
serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu wanatarajia kuanzisha
kituo maalumu kwa ajili ya kufundishia somo la tehema kwa walimu pamoja na
wanafunzi ili kuweza kupanua zaidi katika Nyanja ya teknolijia.
“Kwa kweli tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa
kutupatia vifaa hivi vya kompyuta 25 kwa ajili ya shule zetu za sekondari 14,
bah ii itaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuongeza uwezo kwa walimu katika suala
zima la teknolojia pamoja na mawasiliano,”alisema Jokate.
Komputa hizo 25
ambazo zimetolewa kwa shule 14 za Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani
zimenunulia kwa kiasi ya shilingi milioni 43 zitaweza kuwa ni mkombozi
mkubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi katika kusaidia suala zima la teknolojia
pamoja na mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Jokate Mwegelo akizungumza jambo na baadhi ya walimu wa shule za sekondari
hawapo pichani katika halfa hiyoya ugawaji wa kompyuta hizo, (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama wa kwanza kulia akishuhudia ugawaji wa
kompyuta hizo ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa
wote ambapo shule 14 za sekondari zimeweza kunufaika na msaada huo. (PICHA NA
VICTOR MASANGU).
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama wa kwanza kulia akishuhudia ugawaji wa
kompyuta hizo ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa
wote ambapo shule 14 za sekondari zimeweza kunufaika na msaada huo.(PICHA NA
VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment